Ni sawa kwa Nash Mc kukataa chama na umoja wa wasanii

Ni sawa kwa Nash Mc kukataa chama na umoja wa wasanii?

“Asije msanii akaniambia masuala ya umoja sijui chama, Upumbavu wa ukubwani siutaki”

Hayo ni maneno ya Nash Mc ambayo amechapa kutoka kwenye mtandao wa Twitter kupitia ukurasa wake.

Lakini tukirejea hekima za mswahili daima husisitiza umoja ili kuweza kupata haki zenu au kushinda mnachoshindania kwa nyakati hizo.

Mengi ya sanaa sasa hayako sawia kwa upana, na kuyatoa au kuweza kuyashinda ni kuwa pamoja wasanii.

Na sasa tunaona nguvu ndogo ya wasanii wachache mno wakieleza walau kwa upana namna ya jinsi ya biashara ya sanaa ambavyo inakwenda hovyo. (Fedheha)

Na nguvu yao ndogo inafanya wao kutosikilizwa vyema, ni uhalisi wenye uhalisia wa hakika.

Na mswahili hunena yakuwa “Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” Je! Unafikiri ni sawa kwa Nash Mc kukataa umoja huo?.

Maana lengo la wasanii si moja? kwa maana ya utetezi wa haki zao juu ya mbano wa sasa katika mengi ya sanaa.

Sasa kwanini Nash Mc akatae hadharani kiasi hiki? ilihali wajuzi wanaamini uwepo wake utaongeza chachu ya kudai haki kwa mapana yake.

Wajuzi wanaona kwa mapana yakuwa kwa ukubwa wa Nash Mc na misimamo yake hapaswi kuutenga umoja wala chama, bali kusisitiza uwepo.

 

Chapisho la Nash Mc

Ni huensa kuna changamoto nyingi katika chama cha wasanii na umoja wao lakini haipaswi kuzikimbia bali kukaa na kuziweka sawa zilete usawia wa kesho njema.

Hivyo kutangaza hadharani yakuwa hataki umoja na chama ni wazi inaonyesha ni kwa namna gani ana mfadhaiko wa mengi ya sanaa. (Haifai).

Ingawaje wajuzi wanaamini hakuna ulazima wa lazima kwa wasanii kuwa wamoja, lakini “Umoja wa wasanii ndiyo njia” Tafakarii…!!

#TuzungumzeMuziki