Ni safi kuwa na ongezeko la tamasha la Wasafi, lakini je! kutakuwa na mabadiliko?

Ni safi kuwa na ongezeko la tamasha la Wasafi, lakini je! kutakuwa na mabadiliko?

Hivi ni nani mwenye kupenda maendeleo ya wasanii na sanaa zao asiyependa kuona wanakuwa sawa na upana wa majina yao? (Hayupo)

Kadri siku zinavyosonga ndivyo ambavyo uwingi wa matamasha makubwa yanaongezeka. (Hakika)

Na kila ajaye na tamasha lake/lao huweka simamio la ushindani katika matamasha mengi makubwa ambayo yalikuwepo na yapo. (Uhalisia)

Na katika mwanzo wake huanza kwa huruma katika ombi la kufanikiwa kibiashara katika upana wa tamasha. (Husika)

Na hatimaye mara baada ya mafanikio hakika “Katikati huwachanganya na kusahau chanzo” (Naam)

Wasafi Festival ni uzao wa Diamond Platnumz na timu yake ambapo hakika anajua/wanajua changamoto zote za matamasha yote makubwa hapa Tanzania. (Kweli)

Je! Wasafi Festival wataenda na uhalisi wa tofauti ya matamasha makubwa yaliyopo?. Kwa maana ya uhalisi malipo ya chakula, malazi na usafiri? Na kuwepo na malipo yenye ustahili kwa thamani ya msanii husika.

Kusiwe na picha zenye mn’garo na tambo za kujaza uwanja ilihali wasanii wanafadhaika katika usawia wa malipo. (Soni)

Lakini kumbatio la wasanii katika semi yao ya sanaa imezaliwa upya litakuwa na uhalisia? kwa upana wa kuchukua wasanii wenye ujazo wa sanaa pasina hovyo?. (Swali)

Hivyo fanikio litakuwa kubwa na muendelezo wake kama tu Wasafi Festival itazingatia sanaa kwa ujumla na usawia wa malipo kwa msanii katika ujazo kamili. 

Isiwe zile za watangazaji na madj katika kuwapigia simu wasanii eti! una muda uje kusupport? ilihali tamasha limepewa udhamini mpana katika malipo ya yote. (Fedheha)

Ni vyema kujua pia “Atakaye nafasi huipata, ila kuishi katika ukamili ni changamoto”

Hakika salamu zenye ujazo wa hongera zifike kwa Diamond na timu yake nzima. (Pongezi) Na imani yetu haki na uhalisi wa sanaa utakwenda kuonekana. 

#TuzungumzeMuziki