Ni msanii yupi asiyetamani nguvu ya Clouds Media Group?

Ni msanii yupi asiyetamani nguvu ya Clouds Media Group?

Nyakati zote kweli hutuweka huru, na hii ndiyo njia chaguzi yetu sisi Tizneez.

Maoni ni mengi katika mitandao ya kijamii hasa katika ‘Ali Kiba day’ ambapo Clouds Media Group ndiye chanzo cha sikukuu hii ya leo.

Wote hatujui makubaliano ya Ali Kiba na Clouds Media Group katika ‘Ali Kiba Day’. Na huenda yote ya yote ni ‘Mahusiano ya biashara’ katika mlengo wa faida.

Hakika hii ni faida kubwa kwa Ali Kiba kupewa mahojiano katika vipindi zaidi ya 6 katika siku moja.

Na tangu sa 12.00 Asubuhi Ali Kiba amewasili Clouds na atakuwepo mpaka sa 6.00 usiku.

Katika uhalisi wenye uhalisia ni wazi Ali Kiba na uongozi wake wamepata nafasi kubwa mno, ambapo hatudhani kama yupo msanii ambaye hatamani nguvu hii ya leo na ya nyakati zote kutoka kwa Clouds Media Group.

Ni vyema wengi wajue yakuwa “Clouds wanaweza kubadili mbao kuwa dhahabu” Hakika twasema hilo maana tuna hakika nalo.

Na tunakumbuka vyema semi ya mswahili yakuwa “Ukipendwa na mfalme, hakuna raia wa kukusumbua”

Lakini ‘Kiki’ haitaweza kushinda ‘Muziki’, ‘Akili’ na ‘Uzoefu’ tuna hakika

Na ambaye anasema yakuwa Ali Kiba amekosea maana amezindulia Tanzania kinywaji chake, ni wazi amepotoka vyema.

Maana semi kuu yasema “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako” lakini “Nyumbani ndiyo kwenye yote”

Na masikio na macho ya wengi zaidi Clouds Media Group kwa leo hii, wakati katika mitandao yote ya kijamii chanzo cha habari juu ya Ali Kiba ni Clouds.

Ni msanii yupi asiyetamani nguvu hii ya Clouds?

#TuzungumzeMuziki