Ni lini Kassim Mganga atapewa heshima yake?

Ni lini Kassim Mganga atapewa heshima yake?

Waswahili husema “Mwenye kelele hana neno” kwa hakika ni wasanii wengi uwasikiayo si wenye muziki bali kelele nyingi ambazo ukitazama vipawa vyao ni vidogo mno.

Lakini kelele zao huwatisha watu wa Media na mashabiki hivyo kuamini katika kelele zao, na hatimaye kusahau watu wenye muziki kama Kassim Mganga.

Lakini waswahili hawakukosea kusema “Mzoea udalali duka haliwezi”. Wasanii wengi ni wasanii ambao wamezoea kelele za kiki na mengi, hivyo bila kificho kusimama kwenye muziki hawawezi maana si wasanii wa kutegemea kipaji bali kelele nyingi nje ya muziki.

Ukimtazama Kassim Mganga ni msanii ambaye ni yeye na muziki wake na si jambo lingine.

Kwa muziki afanyao ni wazi ni bora kuanzia kwenye tungo, mpangilio wa sauti lakini nidhamu ya Sanaa. Lakini ni nani afunguaye kinywa chake na kusema ubora wa Kassim Mganga?

Ni wakati muafaka sasa kuhubiri juu ya ubora wake lakini ni vyema tuhuburi muziki pekee na sio mambo mengine ambayo hayakuzi Sanaa wali kuipa msaada ila kuongeza upuuzi na kuwapa majina makubwa watu wenye upuuzi Zaidi.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa