Ni kwamba hawaoni kuhusu Ray C, au mpaka afanye lenye hovyo?

Nguvu ya mtandao imerahisha mengi mazuri katika kupata maoni ya wengi juu ya sanaa ya muziki na wasanii wake kwa ujumla. Lakini katika maoni ya wengi kwenda kwa wasanii wengi yanakuwa si katika kutafakari vyema, bali ni kukurupaka na kimbelembele chenye ujuaji ambao hawajui.

Na mswahili hakuacha kunena yakuwa “Mwenye kutafakari ni bora, sio mwenye kukurupuka na kimbelembe bila kutafakari, hakika hana ajualo”. (Fedheha). Na hii tumeoina vyema kwenye hoja ya mkongwe Ray C baada ya kuweka wazi hisia zake juu ya wasanii wengi wa zamani.

Ambapo alieleza yakuwa “Wasanii wengi wa zamani nyimbo zao hupigwa zaidi pale ambapo hukumbwa na mauti, lakini katika siku za kawaida huwa kawaida” Katika upana ni kawaida msanii yoyote yule akifa nyimbo zake kupigwa zaidi, na kwenye nchi ambazo zimeendelea kisanaa basi msanii huuza tena album au nyimbo kwa ukubwa tu.

Isipokuwa katika tafakari njema ni namna ya nafasi ya wasanii wengi wakongwe katika ‘Media’ sasa. Wapo ambao hunena hadharani wakongwe wameishiwa, jambo ambalo si kweli.

Wakongwe wanachokosa ni namna ya kazi zao kupewa muda kama kazi za wasanii wengi wapya. Mfano wenye uhalisi na uhalisia ni wimbo wake Ray C na Kaligraph Jones wa ‘Aisee’ hakika ni wimbo mzuri ambao una kila sababu ya kupewa muda, Je!unapewa muda?

Lakini laiti kama angekuwa amekufa au amefanya jambo la hovyo hakika lingezumziwa katika vipindi vyote, tena kwa upana. Lakini vipi wimbo wake wa sasa? haufai kuzungumzwa kwa upana? Ipi ni changamoto ya kuuzungumza?

Na kizazi kipya cha watu wa ‘Media’ haipaswi kuzungumza dhihaka juu ya wakongwe maana kwa nafasi yao muda wao ndiyo wachonga barabara katika faida ya muziki wa sasa.

Lakini tusishangazwe mno na kizazi cha sasa kilichojivika ujuzi wa na kutokujua thamani ya msanii/wasanii wakongwe. Maana hata mswahili hunena yakuwa “Uzuri w a mkakaya ndani kipande cha mti” Tafakari..