“Ni fedheha Witnes kufadhaishwa na ukweli aujuao”

“Ni fedheha Witnes kufadhaishwa na ukweli aujuao”

Witnes Kibonge Mwepesi ni jina kubwa na maarufu katika muziki wa hiphop, ambaye pia ni miongoni mwa wasanii wachache na wa kike pekee walioweza kutambulika vyema nje ya Tanzania.

Ni siku kadhaa zimepita tangu pale alipoweka posti yake katika mtandao wa picha ‘Instagram’ ambayo alionyesha kulalama mbele ya mashabiki lakini mbele ya watu wa Media ambao wamekuwa wakitaka awape rushwa ya ngono ili waweze kumpa nafasi katika muziki.

Lakini licha ya kujua ukweli kwenye nafsi yake yakuwa ni nani na nani ambao wamekuwa wakihitaji rushwa hiyo ya ngono hakuweza kuweka hadharani, hivyo mashabiki wamekuwa ni wenye hisia na watu wengi wa Media.

Ni wazi hii ni fedheha kwake yeye maana ni wazi inaonyesha namna ukweli ambavyo umefadhaisha kiasi cha yeye kushindwa kusema hadharani ukweli huo.

Katika uhalisia jambo hili halitaweza kuisha kwake na wasanii wengine wa kike kama tu atakuwa ni muoga wa kuweka ukweli hadharani.

Na nyakati zote “Ukweli utakuweka huru” Hivyo ni vyema Witnes kutafakari katika kuweka wazi ukweli katika mlengo wa kujenga Zaidi muziki huu.

Na katika ile kweli malalamiko pekee hayawezi kusaidia bali ukweli na namna ya wahusika kujulikana katika kujenga na kuondoa swala hili chafu na lenye fedheha.

Na waswahili husema “Akutendaye mtende, usimche asiyekutenda” lakini waswahili waliongeza kwa kusema “Akuanzaye mmalize”

Vivyo yapasa Witnes aweke wazi, ila kama ataendelea kuwa kimya ni wazi hali hii ya uoga itamtafuna na kumeza kabisa muziki wake.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa