Ni aibu Young Killer kuweka wimbo wake kwenye channel ya Harmonize

Ni aibu Young Killer kuweka wimbo wake kwenye channel ya Harmonize.
Wakati wote ndugu zetu “Shahidi ndiye mwenye neno” na hatupi shida kuhubiri yenye mema katika kujenga vyema wasanii na muziki kwa ujumla.
Young Killer ni moja kati ya wasanii bora wa hiphop ambao tumebalikiwa vyema kuwa nao kwenye muziki wa kizazi kipya. Na sisi ni miongoni mwa wengi ambao tunajivunia uwepo wake.
#TuzungumzeMuziki ni kauli mbiu yetu ambayo tumeamua kuishi ndani yake.
Ni wazi swala la Young Killer kuweka wimbo wake wa Unaionaje kwenye akaunti ya Youtube ya Harmonize ni wazi ni jambo la aibu. Ni aibu kwa majibu ambayo alitupa Tizneez mara baada ya kuhoji juu ya yeye kuweka wimbo huo kuwa chini ya Harmonize kwenye mtandao wa Youtube.
Young Killer alisema “Youtube haijawahi kunipa hela tangu kuanza muziki, so nimeamua kuweka kwake ili niweze kupata hela”
Mbali na Young Killer wapo baadhi ya wasanii wakubwa ambao walikiri kuwa na uelewa mdogo kuhusu Youtube na biashara ya katika mitandao kwa ujumla.
Lakini ndugu zetu yapasa mjue Youtube hawatoi tu hela mara unapoweka wimbo wako kwenye mtandao huo, bali ni lazima ufuate taratibu zao ili uweze kupokea malipo mara pale inapostahili kupokea.
Lakini katika uhalisia ni wazi kila msanii anaweza kufanya mtandao wa Youtube kuweza kuingiza hela. Lakini ni lazima ufuate utaratibu na wala si kwa wasanii Fulani kama ambavyo wengi hudhani.
Jambo la Young Killer kuweka wimbo wake kwa Harmonize ni jambo la aibu lakini fedheha, kwa maana ana uhakika gani wa Harmonize kuweza kumpatia malipo yake yakiwa sawa? Lakini anajua kama kazi hiyo itaishia milele? Hivyo malipo yataendelea milele kwa Harmonize, je!yeye Young Killer na uzao wake watafaidika nini miaka ya baadae?
Ni vyema kutafakari haya katika wakati huu maana nyakati hizi zilizo sio nyakati zijazo.
Lakini ni wazi inaonyesha jinsi uongozi wa Harmonize walivyojua maana halisi ya msemo huu yakuwa “Usimuamshe aliyelala” maana ni wazi kama ni lengo la kumsaidia Young Killer wangeweza kumuelekeza njia halali za kuweza kupata malipo yake kazi zake kupitia mtandao huo.
Ila ubinafsi ulichukua nafasi yake, lakini kama Tizneez Media Group tunaweka wazi yakuwa elimu ya kuweza kufanya msanii/wasanii kulipwa kupitia kazi zao wawekazo kwenye mtandao wa Youtube tunayo.
Hivyo kama msanii hufaidiki na Youtube tafadhali tuwasiliane hapa tizneez@gmail.com.

Na wakati wote “Mbinu hufuata mwendo”

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa