Nguvu iliyotumika kusema mabaya ya Ferooz itumike sasa kwenye uzuri wake

Nguvu iliyotumika kusema mabaya ya Ferooz itumike sasa kwenye uzuri wake.

Sijui tunaishi katika dunia ya aina gani katika muziki wa kizazi kipya, kwa maana walio na nguvu ya kusema wakati wote hupenda kuhubiri mabaya Zaidi na sio mazuri yenye maana kubwa kwenye maisha ya msanii husika ya kila leo.

Lakini katika wakubwa wengi kwenye muziki wa kizazi kipya ambao ni wahubiri wema wa mabaya Zaidi ya wasanii yapasa tusiwashangae kwa maana ya wengi wao ni “Uzuri wa godoro wa nje tu, kwa ndani mna pamba” (Akili).

Ni vyema kuwa na nguvu ya kuzungumza yaliyomema ambayo yanajenga Zaidi Sanaa sio mengi mabaya ambayo ni wazi hayajengi Sanaa wala kumjenga msanii.

Ni wazi wimbo wa Ferooz ni wimbo mzuri ambao umebeba ujumbe wenye maana kubwa mno kwenye maisha ya kila mmoja lakini hata kwa upande wake.

Lakini haitashangaza wale ambao wakati wote ni wahubiri wema wa mabaya kukaa kimya katika jambo jema hili la wimbo mzuri, lakini kufungua vinywa vyao katika mengi ambayo hayana faida yoyote kwa msanii kama  Ferooz.

Ni wazi hakuna kingine anachohitaji Ferooz kama kuzungumziwa kwa kazi yake hii mpya na Sanaa yake kwa ujumla na sio habari nyingine mbaya.

Katika miaka miwili nyuma kumezungumzwa mengi juu ya Ferooz ambayo ni katika mlango wa ubaya Zaidi. Na nguvu kubwa imetumika katika kuzungumza hayo, hivyo ni vyema nguvu hiyo itumike tena kuzungumza juu ya kazi yake mpya hii ila kujenga Zaidi Sanaa yake.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa