“Nguvu iliyotumika kusema mabaya ya Chid Benz, itumike tena kusema mazuri yake sasa”

“Nguvu iliyotumika kusema mabaya ya Chid Benz, itumike tena kusema mazuri yake sasa”

Hakuna haja ya kuuma maneno katika kupeana ile kweli yenye kuleta uhuru katika maisha yetu ya muziki wa kizazi kipya. Licha ya uhalisia maisha ya kwenye muziki wa kizazi kipya yamejaa uongo ambao unaaminika kuwa ndiyo ukweli.

Na uhalisia mwingine ni juu ya wahubiri wa Media ni namna ya kuzungumza mabaya Zaidi kwa urefu na ufafanuzi mwema ila ukweli na mambo ya maana kupewa kisogo. Huku wenyewe wakiamini jambo baya ndiyo husikilizwa vyema, ila uhalisia sio kweli bali watu husikiliza maana hakuna cha kusikiliza.

Jambo hili si jambo jema, na jambo hili limeendelea kuwatumbukiza shimoni wasanii wengi ambao kwa bahati mbaya walipata matatizo tofauti tofauti katika muziki wa kizazi kipya, ilihali uwezo wao kuwa mkubwa katika ufanyaji wa kazi.

Kejeli na dhihaka zilitawala mno  juu ya Chid Benz katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma. Kila mtu alisema lake, walioandika kila mtu aliandika lake lakini pia watu wa media waliongea kwa namna wanavyoweza kwa upana wa kuelezea mabaya yake juu ya matumizi ya dawa za kulevya. Ila ni katika mtindo wa dhihaka na kejeli.

Maana ya kusema kejeli na dhihaka ni namna ya watu hawa walivyokuwa wakitumia nguvu na muda kusambaza video za Chid Benz akiwa katika hali isiyofaa, ila sikuona maana ya kusambaza video hizo. Maana hakuna msaada kwa upande wa Chid Benz katika usambazaji wa video hizo ila kuzidisha tatizo kwa mhusika kwa namna ya kujiona hafai tena mbele ya jamii.

Ila jamii inapaswa ijue “Yaliopita si ndwele tugange yajayo” tuna kila sababu ya kuishi katika maneno haya.

Chid Benz alianguka na sasa ameamka tena na nguvu mpya. Nguvu hii sio nguvu ile ambayo ilitengenezwa baada ya kutoka Bagamoyo akiambatana na Babu tale bali nguvu hii ni ya kutoka katika moyo wake mwenyewe.

Kwa maana dawa ya Chid Benz alikuwa nayo Chid Benz mwenyewe. Na sasa amegundua hilo na hakuna sababu ya kuacha kumpongeza kwa maamuzi mema yenye ukombozi katika maisha yake yote.

Hakuna kingine anachotaka Chid Benz Zaidi ya kupewa nafasi tena katika vyombo vya habari. Chid Benz anahitaji nguvu kubwa ambayo itaweza kumfanya ajisikie faraja kama bado ni msanii mwenye kuthaminika.

Ila kasumba ya watangazaji sasa ya kupenda kuzungumzia mabaya tu, hakika hii ni kasumba mbaya mno.

Jema ambalo amefanya Chid Benz la kutoa wimbo ambao umebeba uhalisia wa maisha yake ni jambo kubwa. Ni wazi amejutia muda ambao amepoteza hivyo ni vyema kumpa ushirikiano katika wimbo wake huu.

Tususubiri kuzungumzia mabaya kwa nguvu kubwa hata hili jema tuzungumzie katika nguvu kubwa pia.

Pongezi kwa Q chilla kwa kutendea haki wimbo huu, ambao ni wazi ameimba kwa hisia.

Wimbo huu ni wimbo ambao unagusa maisha ya wengi ambao wamekata tamaa.

“Tuthamini muda huu kwa Chid Benz kabla haujageuka historia”

‘Team Tizneez tunamtakia yaliyomema Chid Benz wakati wote’
Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez