“Ng’ombe akivunjika mguu malishoni hurejea zizini” (Ruby Na Clouds Media Group)

“Ng’ombe akivunjika mguu malishoni hurejea zizini” (Ruby Na Clouds Media Group)

Waswahili husema “Moto ukizimika majivu hayana thamani” Bila kupepesa macho wala kuuma maneno ni wazi Ruby ni msanii ambaye amezimika na majivu yake hayana thamani kwa maana ya nyimbo zake nzuri za wakati uliopita.

Ni wazi Ruby ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu. Lakini ukubwa wa kipaji yapasa uende sawa na kasi ya matangazo ya media ili aweze kufaidika na kazi zake.

Katika uhalisia biashara inahitaji matangazo wakati wote. Ruby ni bidhaa bora iliyokosa matangazo hivyo kadri siku zinavyokwenda tunaona kwa namna bidhaa mbovu zenye matangazo yakutosha kuonekana bora.

Katika ile kweli miaka miwili nyuma Ruby aliweza kuishutumu Clouds Media Group yakuwa hawajampa maslahi yake katika baadhi ya kazi alizofanya nao lakini hata katika shoo ya Fiesta ambayo ilikuwa yafuata kwa wakati huo hawakuwa tayari kumpa maslahi yake stahiki bali finyu. Hivyo Ruby aligomea kushiriki katika tamasha hilo, lakini baadae kukosa kabisa nafasi kabisa kwa upande wa Clouds Media Group.

Na tangu hapo ni wazi hakukuwa na ufanyaji wa kazi yoyote kati ya Ruby na Clouds Media Group.

Lakini ikumbukwe Ruby ni zao la Clouds Media Group, kipaji chake kilitambulika tokea hapo. Na ndipo Media nyingine zikaanza kumfahamu na kuanza kufanya nae kazi.

Tangu Ruby aache kufanya kazi na Clouds Media Group ni wazi muziki wake umeporomoka licha ya baadhi ya Media kujaribu kumsimamia katika kazi lakini pumzi zao zilikata mapema.

Ni wazi kwenye swala la biashara ya matangazo katika kumtangaza msanii ili afahamike ni wazi Clouds Media Group hilo wamebarikiwa. Hivyo wanahaki ya kujisifu yakuwa “Wakianzisha wanafuata”

Ni kosa kubwa kwa kipaji kama Ruby kupita kama upepo, ni wazi yafaa kurudi zizini Clouds Media Group na kumaliza tofauti zao ilihali tuendele kuwa na wasanii wengi wenye vipaji ambavyo vitaendelea kukuza zaidi na kueneza muziki wetu wa kizazi kipya.

Lakin yafaa Clouds Media Group wajue na wajitafakari kwa maana ya “Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama”
#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa