Ndivyo ipasavyo afanyavyo Ray Vany (Wcb)

Ndivyo ipasavyo afanyavyo Ray Vany (Wcb)

Kunako toleo la wimbo wa ‘Chombo’ wengi hawakutilia maanani katika masikio yao, maana inaonekana ni katika fanano la Soco ya Wizkid.

Pamba ziliziba masikio ya Ray Vany na kuendelea na kile ambacho yeye alikuwa akiamini yakuwa ipo tofauti ya Soco na Chombo.

Na uwekezaji wa nguvu ya matangazo kwa hali ya ukubwa ndiyo ambayo ilifuata.

Na nyakati zote husisitiza yakuwa ‘Biashara ni matangazo’ lazima ufanye matangazo mengi kwa upana wa bidhaa uliyonayo kwa nyakati hizo.

Na Ray amejua namna ya nini anapaswa kufanya juu ya bidhaa ya ‘Chombo’. Na tokeo ni kuwa bidhaa imeweza kushika vyema kila
kona.

Ndiyo ipasavyo kwa nyakati kamili, yani ipe nafasi bidhaa yako kwa nyakati sahihi. Sio una bidhaa hii na unazungumzia bidhaa nyingine eidha ijayo au iliyopita. (Haifai).

‘Chombo’ imekuwa kubwa tofauti na dhanio la wengi mwanzoni yakuwa haiwezi kufanya vyema kwa mfanano, lakini ‘matangazo’ yamebadili matokeo.

Hakika ndivyo ipasavyo kwa muenendo halisi wa aina ya Ray Vany.

#TuzungumzeMuziki