Navy Kenzo na Sallam Sk ni mgongano wa kimaslahi kwa Ay na Diamond Platnumz na genge la Wcb.

Navy Kenzo na Sallam Sk ni mgongano wa kimaslahi kwa Ay na Diamond Platnumz na genge la Wcb.

Daima mlete mtu katika njia iliyojaa uzuri katika endelezo jema la jambo afanyalo, ingawaje nyakati nyingine huwa chukizo katika elekezo la njia.

Lakini hatupaswi acha kuelekeza vyema katika ujazo wa kujenga nyumba imara. (Uhalisi).

Mwenye usafi wa moyo basi hata kinywa chake uhubiri kweli yenye kweli nyakati zote, na hofu huivua na kuitupilia mbali katika simamio la ukweli.

Ni wazi katika kweli Navy Kenzo ni moja ya genge bora na zuri ambalo tumebalikiwa kuwa nalo katika muziki wetu.

Hatua zao ndefu na za haraka katika muziki zimefanya ndani na nje ya nchi watu wawafahamu vyema.

Na katika hatua zao za mwanzo walisimama wenyewe kwa maana ya Aika na Nahreel (NavyKenzo). Lakini sasa wapo katika simamio la Sallam Sk.

Ingawaje haijawahi kuwa wazi yakuwa Sallam Sk anasimama kama nani bali ‘Meneja’. Lakini katika uhalisi wa uhalisia kutakuwa na mgongano wa maslahi kati ya Ay, Diamond na genge la Wcb kwa ujumla.

Tuwe wa kweli kipaumbele cha Sallam Sk kinaweza kuwa Navy Kenzo? kulinganisha na Diamond?, na upana wa Ay ukoje?, Je! tafakuri ya genge la Wcb nayo iko kwa namna ipi?.

Ni wazi mgongano wa kimaslahi ni katika upana mkubwa, Je! Sallam Sk anapataje muda wa kuweza kupanga mipango ya kila msanii na mambo yake katika upekee wake?

Urahisi ungelikuwa ni katika muundo wa kampuni hivyo wasanii kila mmoja angekuwa na ‘meneja’ wake si Sallam Sk pekee.

Hapo pasingekuwa na mgongano wa kimaslahi maana kila ‘meneja’ angelikuwa ni mwenye mipango yake katika uuzo wa bidhaa ya msanii wake katika nyakati halisi.

Lakini usimamio wa Sallam Sk pekee anaweza kuuza bidhaa ambazo zinafanana katika nyakati mosi?

Ni wazi lazima endelezo la mgongano wa maslahi liwepo kwa mapana yake, hivyo kuna kila sababu ya Navy Kenzo kujitafakari katika hilo kabla ya ujio wa nyakati ngumu.

Na nyakati zote “Uketipo kwa chakula na mtawala, mtazame vyema aliyeoko mbele yako” Tafakari…

#TuzungumzeMuziki