Nash Mc atashiriki kwenye matamasha mawili makubwa nchini Ujerumani.

Nash Mc atashiriki kwenye matamasha mawili makubwa nchini Ujerumani.

Wenye pakunenea pakubwa daima huendelea kuhubiri ongo ambayo wengi sasa wanaamini yakuwa Nash Mc si chochote wala lolote kwenye muziki.

Lakini wajuzi wa muziki hunena hadharani tena bila uficho yakuwa Nash Mc ni bora katika ubora wa nyakati zote.

Na hii ni katika ujazo wa tungo zenye uhalisi wa kugusa maisha ya wengi katika kila iitwapo siku.

Lakini misimamo ya simamio la mengi yenye haki yake ya sanaa yake na sanaa kwa ujumla bila kujali utumwa wa tangazo kubwa la Radio na Runinga ni ongeza la heshima kwa wajuzi wa muziki.

Na leo hii Nash Mc yuko nchini Ujerumani katika matamasha mawili makubwa ambapo ni Afrikan Festival katika mji wa Tubingen kuanzia tarehe 9 mpaka 12.

Na baadae mji wa Berlin katika tamasha la Rap For Refugees. Hivyo Nash Mc atakuwa nchini Ujerumani kwa takribani mwezi mosi.

Nash Mc wakilisha vyema huko, sisi tunaamini juu ya wewe katika mengi yenye uhalisi wa muziki huu.

#TuzungumzeMuziki