Nani kasema wimbo wa ‘Mbio’ wa Ali Kiba ni mbaya? (Mpuuzeni)

Nani kasema wimbo wa ‘Mbio’ wa Ali Kiba ni mbaya? (Mpuuzeni)

Mitandao imeleta mambo leo katika kila mmoja kuwa mjuzi katika yote, lakini katika uhalisi wenye ujuzi wa mengi katika muziki ni wachache mno. (Naam)

Wengi wao ni katika hisia zao ndani yao si hisia za kimuziki na ujuzi imara. Na ujuzi imara katika muziki ni vyema kujua upana wa muziki wenyewe katika chambuzi si hisia zako bali za upana wa muziki. (Ukamili)

Na daima mswahili hunena yakuwa “Mwenye kelele hana neno” naam ndiyo na ndivyo ilivyo. Kelele za watu ambao si wajuzi wa muziki ni nyingi mno na hawa wamejiweka katika kivuli cha uchambuzi wa muziki na wamepewa vyeo kabisa vya uchambuzi wa muziki. (Soni)

Na kama ukihojia katika ulizo la swali juu ya wachambuzi hawa yakuwa “Ukisema wimbo wa ‘mbio’ wa ni mbaya ubaya wake ni upi?. Hakika majibu yao utasikia hauna vibe, vibe ndiyo nini katika upana wa muziki? (Chekesho)

Hakuna uhalisi wenye uhalisia wowote katika ukamili wa wimbo na ubora wake juu ya kitu kinachosemwa ‘Vibe’ bali ukamili wa wimbo ni katika jazo imara la wimbo. (Hakika)

Na wimbo kamili katika ubora tazamo kuu huwa ni mashairi kwa maana ndiyo nguzo kuu, lakini mdundo katika mapigo ya ala katika endelezo la wimbo, ila uimbaji wa msanii katika sauti yake yenye uhalisi. (Ndiyo)

Wimbo wa ‘Mbio’ umekaa katika ukamilli huo, na hakika ni katika utatu wa wimbo kwa maana waweza kusikiliza katika usikivu wa kwenda kazini, kutoka kazini au katika upana wa mahala pa starehe lakini hata katika faraja ya kufanya kazi kulingana na kazi yako.(Burudani)

Na tunapenda tuwakumbusha kumbukumbu yakuwa ubaya wa wimbo ni katika upana wa mashairi, uimbaji na hata upigaji mbaya wa ala. Lakini uhalisi wimbo wa ‘Mbio’ umekamilika katika ukamili wenye ubora. (Hakika)

#MuzikiNiSisi