Nani alaumiwe kati ya uongozi wa Darasa na Darasa mwenyewe?

Nani alaumiwe kati ya uongozi wa Darasa na Darasa mwenyewe?

Muziki ni wimbo wake ambao ulifanya kila sikio lenye kusikia kuweza kusikia wimbo wake huo.

Huku wengine wakidhani ni mpya lakini ni wazi Darasa alikuwepo kwa muda mrefu kwenye muziki huu. Na sikati tamaa ndiyo wimbo wake ambao ulimtambulisha vyema.

Na mwaka 2016 na 2017 ni miaka ambayo kwa Darasa imekuwa yenye neema katika muziki kwa kuweza kupata mafanikio makubwa ndani ya muziki na nje ya muziki.

Ingawa kwa mwaka 2017 hakuweza kuwa bora Zaidi licha ya kuendelea kutoa nyimbo nyingi na nzuri.

Lakini ukimya wa Darasa katika mitandao ya kijamii unatia shaka juu ya Sanaa yake ya muziki kwa namna ya kuwa kuwa kimya tangu tarehe 21/8/2017 mpaka leo hii tarehe 18/1/2018.

Ni wazi njia ya moja wapo na kubwa katika kusukuma muziki wa msanii kwa sasa ni matumizi ya mitandao ya kijamii.

Na kupitia mitandao ya kijamii tumeona ambavyo wasanii wamekuwa wakipata nafasi za kutangaza makampuni mbalimbali, je!ukimya wa Darasa katika mitandao ya kijamii kuna kampuni ambayo itataka ifanye nae kazi katika ngazi ya mtandao? Ni wazi hakuna kwa maana makampuni hutazama msanii ambaye yupo vyema katika mitandao ya kijamii.

Lakini ukimya wake unazidii kumpotezea mashabiki wengi ambao walimfuata katika mitandao ya kijamii baada ya kutoa wimbo wa muziki, hivyo kitendo cha kuwa kimya ni wazi wanaona hakuna cha maana juu ya msanii huyo.

Ni nani ambaye amempa ushauri wa kuwa kimya kwenye mitandao ya kijamii? Ni yeye mwenyewe au uongozi wake?

Ni wazi yafaa ajue “Wakati wa hari, watu hugombea kisima kimoja”

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa