Nandy vaa viatu vya Vannesa Mdee uende zako.

Nandy vaa viatu vya Vannesa Mdee uende zako.

Unasubiri nini Nandy? hili swali ni rudio mara nyingi katika vichwa vyetu maana daima ”Nyakati hupita”.

Ukimtoa Vannesa Mdee sasa msanii pendwa na kizazi cha mtandao ni Nandy. Na nguvu yake si ndogo ni kubwa katika upana wa majukwaa mengi.

Na hata neno kuu lanena “Enenda pamoja na mwenye hekima, nawe utakuwa na hekima”.

Sasa Nandy anasubiri nini kuvaa viatu vya Vannesa Mdee katika kuwa na tamasha lake la kupita Mkoa kwa Mkoa ili kuweka mizizi imara ya muziki wake?

Maana pia “Alimaye shamba lake atavuna zaidi” Nandy hizi ni nyakati kamili za kuvaa viatu vya Vannesa Mdee katika kamilisho la kupata ziada tofauti na shoo ya kusubiri simu ya promota.

Nandy yukatika ujazo kamili wa kufanya matamasha yake sasa, maana akisema kesho ndiyo iwe hakika hakuna ajuaye kesho.

Nyakati nzuri ni hizi ambazo nguvu yake ikatika ukubwa, hakuna cha kusubiri zaidi ya kuvaa viatu vya Vannesa Mdee na kuanza safari.

Hakika Nandy vaa viatu hivi vya Vannesa Mdee, tena funga kamba kwa upana na nguvu, hakuna cha kusubiri sasa.

#TuzungumzeMuziki