Nandy ni nafasi gani unatoa kwa watunzi?

Nandy ni nafasi gani unatoa kwa watunzi?

Kweli humuweka mtu huru daima, tumekuwa na usikivu mzuri wa kipindi cha Ladha 3600 cha kituo cha Efm ambacho kinaongozwa na Jabir Saleh.

Ambapo Nandy amekiri yakuwa “yeye ni msanii mwenye kutungiwa nyimbo zake zote, na lengo ni kuwapa nafasi watu wengine”.

Hivi ni nafasi gani ambayo anaizungumzia Nandy?. Maana katika uhalisi thamani ya watunzi mpaka sasa haipo.

Lakini licha ya thamani kwa upana wa heshima kwa kazi ngumu ya utunzi lakini mafanikio ya utunzi wao iko wapi kwa watunzi?.

Ikumbukwe uzao wa nyimbo ni wazo ambapo wazo hupelekea mtunzi kutunga kwa maana ya kuandika mistari/mashairi.

Na wapo wenye utunzi wa kutunga na kutengeza mitambao kwa nyakati mosi, na uhalisi si kazi rahisi kama tazamo la wengi wafikiriavyo.

Na mpaka leo hakuna thamani wala heshima ya mtunzi katika uwanja wa muziki, Je! Nandy yeye anatoa nafasi gani kwa watunzi katika semi yake ya leo?.

Uhalisi wenye uhalisia Nandy amepata mafanikio makubwa kupitia muziki wake, sasa nafasi gani ambayo anasema anatoa kwa watunzi wa nyimbo zake?

Kuna mtunzi wa muziki wa kizazi kipya mwenye mafanikio yenye robo tatu ya Nandy?.

Sasa nafasi ipo ataoyo kwa watunzi? au ni semi tu zimemtoka bila tafakari pana ya kufikirika?

Yafaa ifike mahala watunzi wapewe heshima yao lakini thamani ya kazi iende sawia na utunzi wake katika uzao kamili wa wimbo.

Na isiwe ni kunena nyuma ya kipaza ilihali uhalisia wa maisha ya mtunzi ungali katika ugumu na bure yenye fedheha.

Na watunzi ni vyema muamke kifikra sifa isiwe ndiyo mshahara wenu bali fedha yenye mafanikio kamili kwa usawia wa msanii.

#TuzungumzeMuziki