Nandy hakupaswa kumjibu Dudu Baya hata kwa udogo.

Nandy hakupaswa kumjibu Dudu Baya hata kwa udogo.

Kwani kila kitu ni cha kujibu? Tunapaswa kujibu kama yana maana na ni kwa mtu wa maaana mwenye kujua maana. (Si Dudu Baya)

Maana kunena ya hovyo katika mtandao ndiyo yawezayo kumpa Dudu kula kwake, hivyo unataraji majibu ya Nandy yatamfanya Dudu Baya kujua uthamani wa maana katika utu? (Thubutu)

Na neno kuu lanena yakuwa “Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania, usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye mwenzako atakapokuwa amekuabisha” (Naam)

Hakika Nandy hakupaswa kuandika katika kuonyesha maumivu yake kwa posti ya Dudu Baya ambayo imempa fedheha Nandy. Alipaswa akae kimya katika endelezo la kazi zake. (Kabisa)

Kitendo cha kuandika yakuwa ameumizwa na dhalilisho la Dudu Baya linampa nguvu Dudu Baya katika endelezo jema la kumdhalilisha zaidi na zaidi. (Uhalisia)

Ambacho alikuwa anatakiwa kufanya Nandy ni kuidharau aibu kwa upana mkubwa, kwa maana yaliyopita yamepita. Unawezaje kuumizwa tena katika fedheha ambayo imeshapita? (Ajabu)

Na zaidi hupaswi kuonyesha udhaifu wako kwa maana daima ambao wamekosa soni watakuwa wakigusa udhaifu huo katika maumivu juu yako kila iitwapo leo. (Eeh)

Lakini daima Nandy unapaswa kujua yakuwa “Utu busara, ujinga hasara” ukimuacha Dudu Baya na hasara yake utakuwa huna ambacho umepoteza. (Faida)

Kikubwa ni Nandy kuendelea na maisha yake ya muziki yenye mafanikio imara katika pana la songa mbele, kelele za Dudu Baya hazina maana kwake wala faida potezea na dharau kwa mapana. (Hakika)

#MuzikiNiSisi