Namuona Diamond Platnumz ndani ya Harmonize Sehemu ya II

harmonize_ft_diamond_bado video

Makala hii ni mwendelezo wa Sehemu ya I Namuona Harmonize ndani ya Diamond Platnumz

Moyo huficha siri ambazo kwa macho huwezi kuziona, pia kuteleza sio kuanguka mbaya ni kushindwa kunyanyuka tena. Nakumbuka vyema siku ambayo msanii chipukizi Harmonize alipokuwa akitambulisha wimbo wa kwanza Aiyola katika kituo kimoja cha Radio.

Hakika kauli za unyenyekevu zilitawala, haikuwa shida kwa wapenzi wa muziki kutabiri mafaniko zaidi kwa ile nidhamu aliyokuwa ameonyesha siku ya kwanza. Lakini kwa sasa sifikirii kama ilikuwa nidhamu, isipokuwa ugeni na mahojiano pia hakuwa mtu mweye kuamini kwa pale alipokuwa amefika.

“Mwenye sifa yake mpe” si vyema kumnyima mtu sifa yake hata mara moja. Mimi nakupongeza kwa sifa ya kujua jinsi ya kuvaa uhusika wa msanii Diamond Platnumz. Hakika umeweza kwa 70% umebakiza asilimia chache mno uwe Diamond Platnumz.

Sifa ya mashabiki wengi wa sasa ni kusahau mambo mengi yanayokuwa yanatokea kwenye muziki yani katika mlengo wa ubaya au uzuri. Isipokuwa huwa ni wazungumzaji wazuri mara baada ya tukio kutokea tu.

Ni May 2014 ambapo msanii Diamond Platnumz nyota ilitakata zaidi pale ambapo aliweza kuchukua tuzo 7 za KTMA kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake. Na wakati huo akiwa kwenye dimbwi zito la mahaba na mrembo Wema Sepetu ambaye alikuwa ni mrembo wa Tanzania mwaka 2006.

Ni ukweli usiopingika kuwa msanii Diamond Platnumz mahusiano yake na Wema Sepetu yamechangia kwa kiasi kikubwa kufanya umaarufu wa Diamond Platnumz kuwa mkubwa. Ikumbukwe Wema Sepetu ni moja kati ya wadada wenye nguvu zaidi katika magazeti ya udaku ambayo inaaminika ndio magazeti pendwa. Hii inanifanya nijiulize ni kweli watanzania walio wengi wanapenda udaku kuliko mambo ya msingi?

Ni wazi umaarufu wa Diamond Platnumz ulizidi pale ambapo aliamua kufanya mambo ambayo hayakupaswa kufanywa hadharani kwa mila na desturi zetu za Tanzania. Lakini yeye alifanya na Wema na baada ya hapo ilikuwa ni kutawala katika vyombo vya habari katika ngazi zote, kuanzia Blog, Radio, Runinga mpaka magazeti.

Mapema mwaka huu tumeona kile ambacho alikuwa anakifanya msanii Diamond Platnumz akikifanya msanii chipukizi Harmonize. Tukitoa jambo la mahusiano baina yake na msanii toka bongo muvi Wolper ni wazi kumekua na kupitiliza maana ni wazi anafanya kile kile alichokua akifanya bosi wake ili aweze kutawala katika vyombo vya habari.

Ni wazi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa, na hata sasa katika matumbuizo yake amekuwa akienda na msanii huyo wa bongo muvi Wolper. Haikuishia tu katika swala zima la mapenzi yake na Wolper ambao imekuwa ni kama sinema za ngono maana ni wazi wamekuwa wakijionyesha wakifanya vitu ambavyo hatukupaswa kuona kutoka kwao.

Jambo pekee linalofanya nijiulize maswali mengi katika kichwa changu. Je akili ya Wolper ipo sawa?na kama ipo sawa kwanini anafanya vile?alikadhalika kwa msanii chipukizi Harmonize. Na wanafanya kwa faida ya nani? Au wanashindana na nan? Bila kujua kuwa kitu kikikaa kwenye mtandao ni wazi kitaishi milele, Hivyo wanaanda kesho zao za aina gani?

Nani alaumiwe kwenye hili!zaidi ya nafsi zao, pia ikumbukwe alipendalo mtu ni dawa. Ni wiki kadhaa zimepita tena na tukaona video iliyomuonyesha msanii chipukizi Harmonize akiwa na kundi la vijana wenzake wakiongea maneno ambayo ni kejeli kwa aliyekuwa mpenzi wa kupika na kupakuwa wa Diamond Platnuzm mwadada Wema Sepetu.

Jambo pekee ambalo niliwaza ilikuwa ni umri wa Harmonize, kabla ya kufikiri kiwango cha akili yake inapoishia, kabla ya kuwaza mazingira aliyokuwa. Ni wazi amesahau ule msemo wa “Mapenzi hayana dhamana” ikiwa hakuna ajuae kesho hata mtunzi wa kalenda.

Hakika kipande cha video hiyo kimefanya Harmonize azungumziwe zaidi katika vyombo vya habari katika ngazi zote. Hivyo umaarufu wake umeonekana kuimarika, lakini ni ule umaarufu ambapo kimsingi hauji ukiwa na heshima ya kutosha, kama sio kuwa mpumbavu mwenye jina kubwa.

Namuona Harmonize ndani ya Diamond Platnumz

 

>>>Soma muendelezo wa makala hii sehemu ya tatu na ya mwisho>>>

Bongo muvi bongo lala, hii kwa mujibu wa Joh Makin katika wimbo wake wa Manuva, kabla ya Hasi 15 ya nash mc ambapo amesema “Kabla ya mitandao kabla ya wasanii kuanza kulilia likes kabla ya Instagram kuongeza mashoga na malaya wa bongo muvi kuuza sana uroda.

 

www.tizneez.com

Twitter: @ tizneez

Facebook: tizneez

Instagram: @tizneez

Youtube tizneez