Namuona Diamond Platnumz ndani ya Harmonize Sehemu ya III.

13628171_234035143659364_249258339_n

Namuona Diamond Platnumz ndani ya Harmonize Sehemu ya III.

Katika sehemu ya pili ya Makala ya Namuona Diamond Platnumz ndani ya Harmonize  niliandika “Mwenye sifa yake mpe” si vyema kumnyima mtu sifa yake hata mara moja. Mimi nakupongeza Harmonize kwa sifa ya kujua jinsi ya kuvaa uhusika wa msanii Diamond Platnumz. Hakika umeweza kwa 70% umebakiza asilimia chache mno uwe Diamond Platnumz.

Sehemu ya pili ya Makala hii ni sehemu ambayo Harmonize alikuwa ametoa wimbo wa bado na hata kuanza kuweka wazi mahusiano yake na msanii toka bongo muvi anefahamika kwa jina la Wolper.

Inanipa mawazo ya kuwaza kuwa kuiga nacho ni kipaji, maana si jambo dogo kuiga mtu mpaka ukawapa shida wasiojua kutofautisha kuwa huyu ni Diamond Platnumz na huyu ni Harmonize. Inahitaji sikio la ziada wakati ukisikiliza wimbo alioimba Harmonize ili kujua kama sio Diamond Platnumz.

Wapo baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakisema huenda makoo ya yanafanana hivyo swala hilo hupelekea kufanana kwa sauti ya Daimond Platnumz. Lakini je wanajua Harmonize aliwahi kutoa wimbo kabla ya kuwa chini ya Wcb? Na wimbo huo hatukusikia muigo wa msanii Diamond, sasa kipi kinafanya avae viatu vya Diamond  kwasasa katika kila kitu?

Ukweli umepigwa pingu ili uongo uweze kuenea, siwezi kusifu kile anachokifanya Harmonize sasa. Sitaki kuwa katika kundi ambalo haliwezi kusema ukweli ili tujenge wanamuziki wenye ladha tofauti ambazo zitafanya wigo wa muziki wetu utanuke zaidi ya hapa.

Inde ni wimbo uliotoka hivi karibuni  ambao kihalali ni wimbo wa mkongwe Dully Sykes ambaye ameshirikisha Harmonize. Kiukweli nimemuona Diamond ndani ya Harmonize kwa mambo mengi. La kwanza ni kuimba, kiuhalisia ni wazi amefanikiwa kuiga kwa 100%.  lakini ni kwanini ameamua kuwa Diamond wakati bado bosi wake huyo ni msaka tonge tena kwenye huo huo muziki?.Je Harmonize anajitengenezea kesho ya namna gani? Kwani mtu kukuinspire ni mpaka uige kila anachofanya?

Sitaki kuamini kama yeye mwenyewe hajui kama anamuiga Diamond, na kama hajui basi kuna haja ya kuhoji juu ya ustashi wake. Lakini uongozi wake haulioni hili? Je wanafikiri kwa aina hii ya kuiga ataweza kukaa kwenye ramani ya muziki kwa muda mrefu?. Kwanini anaendelea kuiga? Kwanini hafikirii kutengeneza utambulisho wake na aina yake katika kila kitu?, inashangaza kumuona akiwa bize kuiga vitambulishi vya Diamond.

Hoja ya za kipuuzi ni kusema “Harmonize muda mwingi yuko na Diamond hivyo lazima aimbe kama Diamond” Nina kila sababu ya kusema hii ni sababu ya kipuuzi. Huwa napata mashaka kwa wachambuzi na wasanii wakubwa ambao wanaaminika na jamii wakitetea Harmonize kumuiga Diamond huku wakitoa hoja ya kuwa pamoja muda mwingi.

Swala la makundi au wasanii kuwa pamoja muda mrefu wala halikuanza leo wa jana tena ndani ya Tanzania na nje , bali hata muziki ulipotoka huko duniani makundi yalikwepo. Na hata hapa Tanzania makundi pia yalikwepo na umoja wa wasanii ulikuwa ni wa kiwango cha juu.

Tukirudi miaka ya 1990 kulikuwa na makundi kama Tribe X, WWA ikiwa na maana Weusi Wagumu Asilia, Kwanza Unit, na hata miaka ya baadae yani 2000 mpaka 2010 bado makundi yalikwepo kama Ghetto Boyz, Wakali Kwanza, Wagosi wa Kaya na mengine mengi, lakini hakuna mfanano wowote kati ya hao wasanii ambao walikuwa katika kundi moja lakini pia ukaribu wa hali ya juu. Sasa hoja ya kumtetea Harmonize inatoka wapi?

Itaendelea …… Endelea kuwa nasi

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez