Na tumtazame vyema Maasai Prince anacho cha kutangaza nchi yetu kisanaa

Na tumtazame vyema Maasai Prince anacho cha kutangaza nchi yetu kisanaa.

Ili sanaa ya muziki ikue yapasa tupepese macho kila upande ili tuweze kupata watu wenye utofauti wa kuweza kuongeza ushindani katika soko la ndani na nje.

Lakini kubwa ni kutangaza Taifa letu katika tamaduni nzuri kwa njia ya sanaa ya muziki.

Sanaa ya muziki katika upana wake inampa nafasi kubwa msanii mwenye upekee katika kundi la wengi wenye njia moja.

Lakini upekee ni kigezo tu na hakiwezi kukamalika kama hakuna watu wa ‘Media’ ambao watafikisha upekee huo kwa wengi zaidi.

Maasai Prince ni moja kati ya wasanii wenye upekee katika uwanja huu wa muziki, ambapo uwezo wa kuimba lugha tatu unamfanya awe bora zaidi.

Kiswahili, Kingereza na lugha yake ya kimasai inakamilisha utatu wa lugha tatu.

Na hakika ni jambo jema, lakini pia namna anavyoutunza utamaduni wake katika sanaa ya muziki ni vyema zaidi.

Na tungo zake ziko katika ujazo mzuri wa sanaa yenyewe kwa maana ya uelimisho na uburudisho.

Ikimbukwe yakuwa sanaa ya muziki ndiyo sanaa pekee yenye urahisi na wepesi wa kufikisha ujumbe kwa haraka kuliko sanaa yoyote lile.

Na wajuzi wanaamini yakuwa “Muziki unaweza kubadilisha dunia, maana unabadilisha watu”

Hivyo kuna kila sababu ya Maasai Prince kupewa nafasi ilihali aweze kubadilisha mengi katika jamii nyingi.

Naam! nyakati fupi zijazo wimbo wake utatoka, na ni vyema kutazama kwa upana na ukubwa wa kipaji cha msanii kuliko mengi ya nje ya muziki.
#TuzungumzeMuziki