Na tukumbuke kumbukumbu juu ya Langa

Hakika “hakuna mrukaji, aliefauru kuepa kifo” na uhalisi ni kwamba “upweke ni uvundo, ilihali kuondokewa si kwema” fedheha ya kila leo ni kubwa kwa ndugu, jamaa, marafiki lakini mashabiki wa hiphop kwa ujumla.

Hii ni katika kifo cha Langa ambacho kilitokea 13.6.2013 hatimaye leo ni mfanano wa tarehe na mwezi katika kifo chake, ambapo Langa alizaliwa 23.12.1985 Jijini Dar es Salaam, hivyo mpaka anatimiza deni la kifo alikuwa na umri wa miaka 28.

Ilikuwa siku, wiki, mwezi, mwaka sasa miaka 5 tangu kifo chake Langa ambaye sisi tunaamini yakuwa ni moja kati ya wasanii wenye tungo bora zenye uhalisi katika nyakati zote.

2004 ni uchipuo halisi wa Langa katika safari ya muziki wake, na ni katika shindano ya Cocacola Pop Star, ambapo Shaa na Witness walikuwa ni washiriki wenza na “Wakilisha” ndipo ilipozaliwa.

Na kundi la Wakilisha liliweza kutikisa vyema katika uwanja wa muziki na nyimbo ya  Hoi na Kiswanglishi, lakini hakuweza kutoa album. Na baada ya muda Shaa alikacha kundi hilo ingawa Witness na Langa waliendeleza na kuweza kutoa wimbo wa No Chorus, ingawaje hakukuwa na muendelezo tena. (2005)

2006 Langa alitoa wimbo wake wa kwanza kama msani binafsi ambao ni ‘Matawi ya juu’ ambapo audio na video alifanya Teddy Josiah.

Na wimbo huu uliweza kuchukua tuzo ya ‘Kisima Award’ kama wimbo bora kutoka Tanzania Afrika Mashariki.

Nyimbo kama Pipi ya kijiti, Nakotoka, Ganster, Hiphop, Loose you heard, Pesa, Bombaklat, Naposimama, Kifo jela au taasisi, Rafiki wa kweli ni nyimbo zake ambazo wajuzi wanaamini yakuwa ni bora katika nyakati zote.

Na katika ulizo kwa wajuzi wanasema yakuwa “Langa hakuwahi kutoa album ingawaje album yake ipo na ina ujazo wa kazi bora”

Hakika “Mtu atapita isipokuwa muziki” Na wala msifadhaike katika kifo chake maana mswahili anena yakuwa “Kifo na kiumbe, kiumbe na kifo” Ilihali “Hata kufa ni kuishi lakini ni katika kifo”

Maisha mema ya kifo, na wengi wamezoea nena Pumzika kwa Amani, hakika na iwe hivyo kwa Langa.

#TuzungumzeMuziki