Mziki na Ujasiriamali

Sanaa ni hazina na urithi, urithi huu tumeedelea kuupokea kama kijiti kutoka kizazi kimoja mpaka kingine. Ni kitu kizuri kuona mziki unakuwa na kwa kasi, kadri miaka inavyokimbia. Kutoka kuimba kwa kutumia ala za asili kama malimba, zeze na ngoma mpaka sasa ambapo tunatumia ala za kisasa kabisa.

Mziki umekuwa ni kazi na kitega uchumi, ama kwa hakika ukiwekeza katika tasnia hii basi utafaidika na matunda yake. Hili haliwezi kupingika kwa sababu mifano ipo na tunaiona.

Tunaona jinsi mziki ulivyokuwa sekta muhimu katika pato la taifa lakini pia umepunguza kiasi kikkubwa cha watu waliokuwa tegemezi. Vijana kila siku wamekuwa wakijiingiza katika tasnia hii ambayo kama itakukubali basi utadondokea kuwa milionea kama sio bilionea. Lakini kuna swali moja lazima tujiulize, je kila aliyopo kwenye mziki anauhukulia mziki kama kazi? Kwa sababu kupitia mziki tayari tumeshapata makundi kadhaa ya watu ambao ni maproducer, wasanii, madj pamoja na mameneja. Hawa wote wanategemea mziki kuleta chakula katika meza zao.

Lakini sio wote ambao wanauchukulia mziki kama kazi hasa hapo Bongo ambapo wasanii ni wengi lakini wenye kufaidika na mziki ni wachache. Hii inatokana na vitu vichache ambavyo kimtazamo uanweza kukubaliana na mimi. Kwanza kabisa elimu. Tunapozungumzia elimu tunajaribu kufumua kwa mapana yake kama ambavyo wahenga walivyosema kuwa elimu ni bahari. Basi bahari hii kwa kwetu Tanzania wachache ndio wenye uwezo wa kuyaoga maji yake. Elimu imekuwa chanzo kikubwa cha kuwafelisha wasanii wetu. Elimu sio kujua kuandika mashairi au kuwa mhitimu wa vyuo vikuu.

Runapozungumzia elimu katika mziki ni namna ambavyo msanii anauchukulia mziki wake kama biashara nyingine, hicho anakuwa na uelewa juu ya mamabo yafuatayo kuhusu watumiaji wake. Kwanza lazima ujue ni kundi gani la watu unaowatengenezea mziki wako, najua wengi wenu mtasama vijana. Sawa lakini pia lazima ujue jinsi ya kuiteka akili ya kijana kupitia Sanaa yako na ubunifu.

Tatu lazima ujue kijana ni mtu ambaye anakimbizana na ulimwengu katika mambo kadha wa kadha ikiwemo mitindo na teknolojia. Hivyo ili kuhakikisha unaukonga moyo wake hasa katika video zako hakikisha unakuwa umevalia vema na unavutia.

Lakini tukija kwenye teknolojia, zama za CD na DVD zimepitwa na wakati, hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa mziki wako unapatikana katika website mbalimbali za mziki. Lakini Bado tumekuwa na tatizo la wasanii wetu kutokuwa na tovuti zao binafsi ambapo shabiki wake anaweza kuinga na kukuta makusanyo ya kazi zako mbali mbali.

MicrosoftAzure

Pengine wengine wanafikiri kuwa gharama za kuendesha tovuti ni za juu mno, ni kweli lakini siku hizi makampuni yanayotoa huduma hii yapo mengi. Microsoft Azure ni huduma ya server inayotolewa na kampuni kubwa dunia ya Microsoft. Huduma hii itakuwezesha kuhifadhi kumbu kumbu zako kwa uhakika lakini pia inampa mtumiaji wake uwezo wa kuhost website ikiwa na database kwa gharama nafuu kulingana na matumizi yako. Hivyo kama ulikuwa unaogopa gharama za kuhost website Microsoft Azure itakufaa.

office-365

Lakini pia Microsoft imezingatia kuwa kuna shughuli nyingi za kijasiliamali unazoweza kuzifanya ukiwa kama msanii mbali na kuimba tu. Hivyo imekuja na Microsoft Office 365, Programu ambayo inakuwezesha kufanya kazi zako mahali popote ulipo bila kuhitaji kuwa ofisini. Kama msanii unaweza ukawa upo mikoani kwenye matamasha lakini majukumu yako mengine ya ofsini ukawa unayatekeleza bila tatizo lolote. Huduma hii inapatikana kwa gharama nafuu vile vile kulingana na ukubwa wa ofisi yako. Acha kuwa msanii ni wakati wa kutengeneza mkwanja.