‘Myonge mnyongeni haki yake mpeni’ Harmonize

‘Myonge mnyongeni haki yake mpeni’ Harmonize

Mwanzo wake hakika wengi hawakuona kama anaweza kufanya jambo tofauti kwenye muziki huu na kuweza kubaki kama alama.

Kwa maana ya kuwa Diamond wa pili katika mengi yahusuyo muziki. Jambo hili lilikuwa kero na wenye moyo wa kupenda vipaji vipya hawakauweza kufunga vinywa vyao katika kutoa hoja njema za kutaka msanii huyu mchanga abadilike ili apate uhalisia wake.

Ndiyo maana ya Team Tizneez kuandika http://tizneez.com/makala/namuona-harmonize-ndani-ya-diamond-platnumz/

Lakini ni katika kumjenga awe msanii mwenye nafasi yake lakini upekee wenye mafanikio ya kisana na maisha ya kawaida.

Ni wazi kwa sasa Harmonize amekuwa na nyimbo nyingi lakini moja ya nyimbo zake ambazo zitabaki kama alama katika muziki huu ni wimbo wa “Happy Birthday” ambao ni uzao toka Upris Music.

Wimbo huu umekuwa ukitumika kila leo na watu wengi mara tu wanaposherekea kumbukumbu za tarehe na mwezi wa kuzaliwa.

Lakini wapo watu ambao wamekuwa wao hupinga kila wimbo na kusema ni mbaya na hii ni kutokana na hisia hasi ambazo kimsingi hazina maana wala faida kwenye muziki huu.

Katika uhalisia “Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni” ni wazi wimbo wa Happy Birthday utaishi kila leo.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa