Mwezi wa 3 ni mwezi wa majonzi zaidi kwenye utamaduni wa watu wa hiphop Tanzania

Mwezi wa 3 ni mwezi wa majonzi zaidi kwenye utamaduni wa watu wa hiphop Tanzania

Maana moja ya watu ambao walichangia kukua na kuenea kwa hiphop ndani ya nchi lakini nje, ambaye ni Nelson Chrizostom Buchard maarufu Father Nelly alifariki Dunia kwa kuchomwa kisu huko Arusha mwaka 2006.

Father Nelly alikuwa muasisi wa kundi la XPlastaz ambalo ndilo kundi pekee lililotoa msanii aliyeshiriki kwenye Kilinge (Cypher) katika Tuzo za BET (BET AWARDS) 2009.

Ambapo msanii huyo kutoka XPlastaz anaitwa G Son Rutta, na ashiriki katika Cypher hiyo akiwa na wasanii kama Krs One, wale na wengine wengi.Na katika Cypher hiyo G Son alitumia lugha ya kiswahili katika michano yake.

Na tukirudi katika upande wa marehemu Father Nelly wimbo kama Nini Dhambi na Ushanta ni nyimbo ambazo ziliweza kumpa heshima kubwa katika utamaduni wa HipHop.

Father Nelly alizaliwa tarehe 18/2/1976 na kufariki tarehe 29/3/2006. Kwa heshima yake mwezi huu wa tatu tutazungumza mengi mno kuhusu yeye na XPlastaz kwa ujumla.

Na tunafanya haya kwa kuwa Tizneez tumesimama katika kauli yetu ya Lakini hatuwezi kuacha kuzungumza juu ya mkongwe Jcb kutoka Watengwa ambaye alianzisha kampeni ya Arusha Bila Visu Inawezakana.

Na kampeni hii ilikuja baada ya matukio mengi ya vijana kuchomana visu na kukatisha maisha ya vijana wengi.

Pumzika Kwa Amani Father Nelly.