Mwasiti na upana wa simamio la muziki pekee.

Mwasiti na upana wa simamio la muziki pekee.

Daima mtu aliyemakini katika mambo yake ni bora kuliko mwenye upotevu. Maana umakini utamfanya kuwa na endelezo la hekima kila iitwapo leo.

Sisi ni nani kiasi tushindwe kusifu wimbo wa Mwasiti ambao waitwa ‘Mapene’? Hakika yapasa tusifu maana hata mswahili anena yakuwa “Mwenye sifa yake mpe”

Sisi ni waswahili mno hivyo bila kusifu wimbo huu tutakuwa tumeishi nje ya uisho wetu wa mswahili wenye ujuzi mpana wa muziki.

Pongezi zianze kwa Mario ambaye ndiye mtunzi wa tenzi zenye maneno matamu ya kiswahili.

Lakini ni wapi umeona muziki umekamilika bila (Ala)mdundo?. Hakika hakuna. Muziki ni changanyo la sauti yenye tenzi na mdundo, hapo ndipo muziki ukamilikapo.

Mfano wa makopo yadondokavyo katika uzuri, ni uhalisi wa mdundo wa huu wa Kimambo Beats alivyodondosha. Huku sauti ya Mwasiti yenye mkwaruzo ilivyopita juu ya mdundo huu imefanya kuwepo na ukamilisho wa wimbo.

Lakini hatujasahau vinanda venye kusindikiza mdundo na mapito ya malalo juu ya mdundo wa sauti nzuri ya Mwasiti. Hakika changanyo la vyote limeleta yote yenye upana na ubora wa wimbo kamili.

Tunasikia kelele za wengi yakuwa “Wenye kiki ndiyo wanauza” Hivi na kiki zao wanauza nini? na katika nyakati zipi?. (Chekesho)

Je! kiki zitakaa nyakati zote kwenye uisho wa msanii na sanaa yake? Hapana bali muziki wenyewe. Basi Mwasiti simamia simamio
la muziki wako.(Uhalisi)

Wewe ni bidhaa bora katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya, chaguzi lako la upande wa muziki kuliko matendo ni jema na utaishi nalo.

Pongezi zetu ziwe nawe katika wimbo wa ‘Mapene’ umetenda haki ya usikivu katika masikio yetu, hivyo barikiwa na tegemeo la mengi kutoka kwako ni kubwa. Sisi ‘Tunakuaminia’.

#TuzungumzeMuziki