Muziki wa hiphop utafanya vizuri Zaidi mwaka huu 2018.

Muziki wa hiphop utafanya vizuri Zaidi mwaka huu 2018.

Muziki wa hiphop ni muziki ambao miaka kadhaa nyuma umeonekana si muziki wa biashara kama aina nyingine ya muziki kwa hapa nchini kwetu Tanzania.

Ilihali katika ile kweli hakuna muziki usiokuwa biashara nyakati zote. Ni wazi biashara inahitaji matangazo hivyo kwa kuwa muziki wa hiphop ulikosa matangazo ndiyo maana ukaonekana si biashara.

Licha ya kukosa nafasi ya matangazo muziki huu umeendelea kusogea mbele kila leo, ingawa ni kwa ugumu wa hali ya juu.

Mwaka 2018 umeanza na kuona namna ambavyo vituo vya Radio na Runinga kuanza kwa upana kuipa nafasi kwa kusikika vyema kwenye vipindi vingi vya burudani ambavyo havikuwa vinacheza muziki huo walau hata kwa 30%.

Kutokana kuweza kuongeza muda wa kucheza na kuzungumza juu ya muziki wa hiphop ni wazi 2018 utakuwa mwaka mwema maana masikio ya wengi yatasikia vyema habari za muziki huu.

Kikubwa ni wasanii husika kutoa ushirikiano maana iko wazi wasanii wa hiphop kuna wakati wana misimamo isiyo na maana wala faida, hivyo ni vyema kujitafakari katika nafasi hii kubwa ambayo sasa vituo vingi vimeweza wapatia.

 

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa