Muziki umekua kwa wasanii kuendelea kufanya shoo bure za Media?

Muziki umekua kwa wasanii kuendelea kufanya shoo bure za Media?

Wasanii na watangazaji wanahubiri mno yakuwa muziki umekua. Je! Wametafakari kauli hiyo na hali halisi ya uendeshwaji muziki?.

Hivi muziki umekuwa au umekua? Maana wanawezaje kusema muziki umekua wakati Media bado zinawafanyisha wasanii shoo bila malipo? Na ole wake msanii akatae kufanya, basi hapo nyimbo zake zitazimwa kupigwa.

Muziki umekua kwa wasanii kulazimishwa kuposti matangazo ya Radio? Tena kama msanii hajaposti na simu atapigiwa “Mkuu hatuoni tangazo letu”.

Muziki umekua kwa wasanii kutumika kimabavu na viongozi wa juu? na kupangiwa usimposti kiongozi fulani? (Hakuna Uhuru).

Muziki umekua kwa wasanii kuishi kwa kupangiwa maisha mbele ya vipaji vyao? (Mdau). Muziki umekua ilihali msanii asipomposti tu mtangazaji katika mfanano wa tarehe na mwezi wa kuzaliwa kwake hugeuka tatizo?.

Muziki umekua ilihali msanii hawezi kumlipa mtayarishaji wa muziki?. Muziki umekuwa yakuwa yupo mmoja apangae huyu awe chini na huyu awe juu?.

Muziki umekua huku Wasanii hawana sauti mbele ya Media?. Kweli muziki umekua kwa watangazaji kuwa na wasanii wao? (Mameneja).

Muziki umekua ilihali hata hatuna hata tuzo zetu ambazo zinawapa wasanii njia ya kusogea mbele zaidi. Maana waswahili husema “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako”.

Muziki umekua lakini mpaka leo idadi kubwa ya wasanii wanasubiri shoo ya mdau na si kuandaa shoo zao. Sasa hapa muziki umekua nini?.

Ni vyema tuishi katika kweli lakini ambayo mnayahubiri basi tuyaishi katika ile kweli kwa kila mmoja kusimama katika nafasi yake na kufanikiwa (Msanii).

Tukisema muziki umekua yafaa kuwa na usawa katika kila mahala panapohusu muziki, Kwa maana ya uhuru wa kila jambo lakini haki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa