“Muziki pekee hautoshi kwa Aslay”

“Muziki pekee hautoshi kwa Aslay”

Huwezi kutaja wasanii ambao wanafanya vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya bila kutaja jina la Aslay.

Tukitazama katika historia ya muziki Aslay si msanii wa kwanza ambaye ameweza kufanya vyema katika kipindi kifupi. Wasani wengi  walitokea na walipita vyema kama upepo mzuri wa fukwe za bahari ya hindi kwa kukosa akili ya biashara.

Tukisema biashara hapa tunatazama namna ya msanii kutengeneza fedha Zaidi nje ya muziki ili aweze kuendeleza vyema uwekezaji wake katika kazi ya muziki.

Na hapa tunaona ni wazi Aslay anahitaji meneja mwenye utashi wa juu Zaidi wa maono ya uwekezaji mkubwa kutoka kwenye muziki kwa maana ya kuweza kuzifuata kampuni na kufanya msanii wake aweze kuwa balozi wa kampuni husika.

Lakini ni wazi ukitazama uongozi ambao anao ni wazi sio mtu/watu wa kuweza kwenda kuyafanya haya, bali ni uongozi ambao uko kusuburi Zaidi na kuhakikisha radio,runinga na blog zinaendesha vyema muziki wao.

Tukisema muziki umebalika ndiyo maana ya kuwa na meneja ambaye anauwezo wa kuandika jambo na kwenda kuliwakilisha kwa kampuni na kuweza kufanikisha msanii wake ametengeneza fedha ambazo zitaendeleza vyema Sanaa yake kwa ukubwa.

Hivyo Aslay anapaswa kujua muziki huu pekee hautoshi kumfanya aendelee kuwepo ila akili ya biashara yenye uwekezaji mkubwa kwenye muziki kwa hakika itamfanya aendelee kuwepo Zaidi na Zaidi.

Na wakati wote ni vyema ajue “Figa moja haliinjiki chungu”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa