“Muziki na pigo kamili la mashabiki” (Sikitiko)

“Muziki na pigo kamili la mashabiki” (Sikitiko)

Hivi nini wanataka mashabiki walio wengi? tunauliza tena hivi ni nini wanataka?. Mbona hawana nafsi zenye uchungu na muziki?. (Soni)

Nafsi zao zimejaa matendo zaidi na muziki wameupa kisogo, ilihali matendo hupita isipokuwa muziki kamili wenye ujazo. (Uhalisia)

Neno kuu lanena yakuwa “Fumbua kinywa chako na uhukumu kwa haki” Hakika hatuna budi kuinena kweli hadharani bila uficho. (Hukumu)

Na kutumia mfano wenye uhalisia si dhambi bali kweli yenye ujazo halisi na kamili.  Leo hii tumeona Dudu Baya amekuwa kinywani kwa wengi mno.

Na hata katika posti zake za mtandaoni wa picha (Instagram) maoni mengi tawala tena katika uwingi. Lakini hata mahojiano yake ni mengi zaidi. (Eeeh)

Lakini amini tunenayo yakuwa hakuna hata mmoja ambaye anazungumza muziki bali hovyo yenye majibizano ya kuchekesha. (Fedheha)

Na tumewiwa kuwakumbusha kumbukumbu yakuwa 15.6.2018 aliachia kibao chake cha Rimoti akiwa na Much More na Brown Punch. Na tizneez haikuacha kuzungumza wimbo huo. (Kabisa)

Kibao hiki kikapita mithili ya pepo za bahari ya hindi,  na hakuna posti yake katika mtandao iliweza kufikisha hata pongezi 10 tu juu ya wimbo wake. (Fedheha kwa mashabiki)

Lakini leo katika matendo posti yake imekuwa na zaidi ya pongezi zenye hovyo zaidi ya 500 na kuendelea. (Uhalisia)

Sasa wajuzi hawaachi/hatuachi kuhoji yakuwa “Mashabiki wanataka nini? muziki au matendo? Lakini je! matendo yanakuza muziki? (Wapi).

Hakika muziki una pigo kubwa la mashabiki wenye upana wa utambuzi wa muziki. Leo hii stori na neno konki na mbwembwe za Dudu Baya si muziki tena. (Ajabu)

Je! ikipita hii Dudu Baya atazungumziwa kwa lipi?  (Hamna). Sa itakuaje? 

Mashabiki ni sehemu kubwa ya ushusho wa muziki huu, lakini wenyewe hawajali bali kujali kutoa lugha na kushabikia matendo zaidi. (Soni)

Ni vyema mashabiki kuwa na simamio la muziki, matendo yapo lakini isiwe na ugeuzi wa ushabiki kana kwamba ni wimbo. 

Lakini Media na watu wake kusimamia hovyo hakika tutapata hovyo mbaya zaidi na anguko la muziki. Tunapenda kukumbusha tu yakuwa 

 “Enyi wajinga acheni ujinga mkaishi mkaende katika njia yenye ufahamu” (Hakika)

#TuzungumzeMuziki