Muziki haujampita Joslin bali upepo wa kiki na usingizi wa ‘Media’.

Muziki haujampita Joslin bali upepo wa kiki na usingizi wa ‘Media’.

Masikio yetu yamekuwa na usikivu mzuri juu ya album ya ‘Parfume’ toka kwa Joslin, ambayo ilitoka mwaka 2004, na hii ndiyo album ya kwanza ya Joslin.

Na album hii ina nyimbo 12, ambapo baadhi ni Parfume, mshikaji mmoja, Maisha, Simuelewi, Niite basi na nyingine nyingi.

Na album hii ilifanyika chini ya Jonas na Master Jay, na mpaka sasa hakuna takwimu halisi yakuwa iliuza kiasi gani, lakini inaaminika yakuwa ni moja ya album bora za nyakati zote.

Lakini katika ujazo wa album hii hakika inatoa maana na uhalisi wa kipaji cha Joslin katika mapana yake.

Na tumejipa usikivu wa album ‘Parfume’ katika kutaka kujua uhalisi wa baadhi ya watu wenye kunena yakuwa muziki umempita Joslin.

Hakika si kweli muziki haujampita Joslin kama wanenavyo wachache, bali kilichompita na kinachompita Joslin ni kiki na usingizi wa ‘Media’ katika lalio la kutazama mengi ya hovyo ndiyo waweke nguvu katika sanaa ya msanii husika.

Joslin anabaki kuwa bora katika uimbaji na kuchana, na yote anafanya katika usawa na ubora wake.

Na kwa aina ya ladha yake katika album hii hakika alikuwa mbele ya nyakati, hivyo hakuna chenye kumshinda nyakati hizi, bali ‘Kiki’ na ‘Usingizi wa Media’

Na kama ‘Media’ zikiweka uhalisi wenye uhalisia hakika Joslin anaweza kurudi vyema katika soko la muziki na kufanya zaidi ya alivyofanya.

Hakuna chenye upya katika uwanja wa muziki ambacho Joslin atashindwa kwenda nacho kwa usawia kwa maana ya utunzi, uimbaji na kuchana, achilia mbali ‘Kiki’.

#TuzungumzeMuziki