Muziki biashara na Biashara ya muziki.

Muziki biashara na Biashara ya muziki.

Mosi Biashara ni shughuli ama mchakato wa kununua na kuuza mali, vitu au lolote katika uuzaji. 

Biashara yaweza kufanywa na mtu binafsi au ushirikiano wa umoja ama jamiii kadhalika nchi kwa ujumla.

Na biashara zimegawanyika katika nyanja tofauti tofauti. Lakini tazamo letu sisi Tizneez ni Muziki biashara na biashara ya muziki.

Muziki ni biashara yenye ukuu wenye uthamani kila iitwapo leo. Na biashara ya muziki ni yenye kuuzika kila leo katika mengi. 

Kimsingi wasemao yakuwa kuna aina ya muziki si biashara ni wenye kupotoka vyema. kwa maana “Hakuna muziki usiokuwa biashara Duniani”

Na Biashara ya muziki inahitaji akili ya biashara kama biashara nyingine. Na moja ya biashara ya muziki ni upana wa kufanya shoo katika majukwaa tofauti.

Na wapo wasanii ambao wao hukwama katika jukwaa moja kwenda jingine. Na mkwamo wao chanzo kikuu ni ufahamu tu. 

Mfano wapo wasanii waliweza kushiriki Wasafi Festival ya 2018 lakini kwa kupata kwao shoo wakanena mabaya juu ya Fiesta tena kwa uwazi.

Hapo wakaharibu mahusiano ya biashara na waandaji wa Fiesta. Na uhalisia pia wapo ambao walikuwa Fiesta wakanena mabaya juu ya Wasafi Festival mwisho wa siku wakokosa Wasafi Festival.

Sasa wasanii wa namna hii wanaonyesha ni jinsi gani hawajui upana wa biashara. Ilifaa msanii aliyepata Fiesta au Wasafi afanye kwa nafasi yake tu ya biashara yake.

Si kufungua kinywa katika kunena yenye hovyo kwa yoyote yule katika waandaaji wa shoo hizi.

Maana yafaa msanii yeye abaki kati bila egemeo la upande kwa maana ya kuendelea kufanya biashara yake ya muziki kwa ukubwa.

Pongezi kwa wasanii ambao ni wenye ufahamu mkuu katika kufanya biashara yake bila kufungamana na upande wowote ule. 

Soni iwe kwa wasanii ambao wao wamechukua upande na sasa wamekosa kote, ukiwa ni mfanyabiashara ni vyema usifungamane na upande wowote bali biashara yako.

#MuzikiNiSisi