Muunganiko wa Nikk Mbishi, One The Incredible na Stereo ni ujazo kamili wa hiphop Tanzania.

Muunganiko wa Nikk Mbishi, One The Incredible na Stereo ni ujazo kamili wa hiphop Tanzania.

Ni mjuzi yupi asimame hadharani na abishe juu ya ujazo kamili wa ufanyaji wa muziki wa hiphop kwa Nikki Mbishi, One, na Stereo?. Hakika hayupo maana wajuzi wote wanajua uhalisi na uhalisia wa wasanii hawa.

Over and Over ni kazi mosi katika upana wa muunganiko wa ‘Sisi The Trio’. Lakini hampaswi kusahau ‘Classic’ ‘2012-13’ ambapo One, Nikki, na Stereo walikutana humu kwa mapana yao.

Ambapo Fid Q alisimama katika kiitikio, na wajuzi wa muziki wanaamini yakuwa hakuna kingine ambacho Fid Q angeweza kufanya zaidi ya kiitikio tu. (Uhalisi).

Muunganiko wa wasanii wa hiphop kwa sasa umekuwa ni katika endelezo zuri, lakini muunganiko huu ni katika ujazo wa kamili wa hiphop kwa upana wa tungo, mitambao, lakini ladha tamu isiyochosha wala kuboa masikioni. (Hiphop)

Wajuzi wanamini kama kutakuwa na usawia katika muziki wa kizazi kipya hakika kundi hili ndilo litakuwa bora zaidi kuliko mengine. Ingawaje sisi hatupendi kuishi katika uisho wa hisia, hivyo tuko tofauti na wajuzi. (Uhalisi)

Ingawaje tunajua upana wa ujazo wa wakali hawa, ambapo kama uwanja wa muziki ukiwa na usawia hakika kila mmoja atajua kwa mapana yake ukubwa na ujazo halisi wa One, Nikki, na Stereo.

Ni vyema uwanja wa muziki kuwa na usawa katika usawia wa kila upande ili tuweze kupata kumsikia/kuwasikia kila msanii/wasanii kwa mapana yao kwa mlingano wa kazi halisi walizonazo.

#TuzungumzeMuziki