Muda wa dhihaka hauwezi kumsaidia Godzilla bali kumpoteza kabisa.

Muda wa dhihaka hauwezi kumsaidia Godzilla bali kumpoteza kabisa.

Naona wapenzi wa hiphop na wale ambao sio wapenzi wakiwa katika kundi moja la furaha kuona namna ya Wakazi na Godzilla wanavyotupiana maneno kila leo.

Chanzo kikuu cha kutupiana maneno kilianza katika mtandao wa “Twitter”lakini sasa si maneno bali wimbo juu ya wimbo. Wakazi ndiye wa kwanza kutoa wimbo ambao umebeba ujumbe katika kumsema vyema mpinzani wake.

Lakini wimbo huu ni wimbo ambao umeandikwa na kuandaliwa vyema katika kiwango cha juu kwa maana tumeona nyuma ya utayarishaji yupo mkongwe mwenye ujuzi wake Q the Don.

Siachi kusema hii ni miongoni mwa nyimbo bora za ‘Diss track’ nzuri yenye ubora kama kipimo kile cha cha Ant Virus za Vinega.

Wimbo huu umebeba uhalisia wa lile jambo ambalo lilikua linaendelea baina ya Wakazi na Godzilla. Na muda mchache Godzilla aliibuka na kujibu wimbo huo wa Wakazi, lakini katika uhalisia wimbo wake ni wimbo uliochini ya kiwango.

Sisi hatuwezi kuita wimbo kwa maana hauna vigezo stahili na hata ukisikiliza unajua Godzilla amefanya mitindo huru  hakuna alichoandika, lakini kurudia baadhi ya mistari ambayo wiki kadhaa aliimba katika mahojiano yake.

Kwa mantiki hiyo Wakazi ameibuka mbabe na mshindi kwa namna ya maoni katika mitandao ya kijamii.

Swala hili limeamsha muziki kwa namna moja au nyingine lakini uhalisia kwa sasa Wakazi si mtu wa kushindana na Godzilla kwa hali yoyote lazima Wakazi atashinda.

Maana Zilla ni msanii aliyechoka kimawazo na hata ukisikiliza vipindi vya burudani watangazaji wamekua mashabiki wema juu ya Wakazi jambo hili linaendelea kumtafuna vyema Godzilla.  Lakini mfananisho wa Godzilla na Wakazi kutoka kwa watangazaji wa vipindi vya muziki wa kizazi kipya ni mkubwa.

Kuanzia katika ngazi ya mitandao ya kijamii mpaka kwenye vipindi. Ila wamesahau kabisa moja ya chanzo kikuu cha anguko la Godzilla kimuziki ni kufaninishwa na kulinganishwa na Billnass.

Itaendeleaa…..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa