Mtoto wa Dandu ‘Cool James’ chanzo cha ufunguzi wa njia ya muziki kilichosahaulika na wengi.

Mtoto wa Dandu ‘Cool James’ chanzo cha ufunguzi wa njia ya muziki kilichosahaulika na wengi.

Ni nani akumbukaye kumbukumbu zake zaidi ya wajuzi wa muziki?. Hakika hakuna na kwa wajuzi ni chukizo, lakini hawana la kufanya zaidi ya mioyo yao kujaa mfadhaiko tu.

Mtoto wa Dandu ni moja ya wasanii wa muziki ambao wamechonga njia kwa upana kiasi cha mafanikio ya wasanii wengi katika sasa. (Tuzo)

Mtoto wa Dandu alizaliwa mnamo 1970 Jijini Mwanza na 1983 ndipo alipoanza na pilika za muziki.

Swahili Nation akiwa na Andrew Muturi (Kenya) waliweza kuwa na kundi hilo ambapo wimbo wa ‘Mapenzi’ uliweza kufanya wengi kujua upana wa sanaa zao.

Na mwaka 1993 ni uzao wa Dandu Planet nje ya Swahili Nation ambapo Black Teacher ndiye mtu ambaye alikuwa nae.

Ila Dandu Entertaiment 93-20 ni muendelezo kamili katika upana wa muziki wake katika upana wa Afrika Mashariki lakini nchini ‘Sweden’.

Na 1999 ni uzao wa tuzo za ‘TAMA’ yani Tanzania Music Awards. Ambapo wazo kuu na upana wa uanzilishi ni msanii Cool James (Mtoto wa Dandu)

Na miaka michache mbele badiliko likawa ni ‘KTMA’ kwa tafsiri ya Kilimanjaro Music Awards. (Fedheha)

Na hii ilikuja baada ya udhamini wa kinywaji cha Kilimanjaro. Ingawa sasa kuna miaka zaidi ya miwili bila uwepo wa tuzo hizo. (Soni)

Ikumbukwe “Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako” Na Cool James aliweza kutupeleka kwa jirana maana hakika tuzo hizi zilikuwa na nguvu kubwa.

Lakini siasa za siasa zimeleta mauti ya tuzo hizi, ila mauti mengine ni katika utoaji maana lawama nyingi kuliko furaha ya kusaidia kujenga heshima ya msanii husika katika ushindi. (Uhalisi).

Wajuzi wanatujuza yakuwa Cool James alikuwa ni mwenye upana wa mawazo katika endelezo jema la sanaa.

Lakini ‘Kila chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo” ambapo 27.8.2002 Cool James alitimiza kwa nafasi ya nyakati zake. Ajari ya gari ni chanzo cha kifo chake. (Dar es Salaam)

Na nyakati hizo wimbo wake wa sina ‘Makosa’ ndiyo ulikuwa wimbo pendwa zaidi kwa wengi.

Pongezi za wajuzi kwa Marehemu Cool James hazina mfano wake kwa upana wa uchangiaji wa kukua na kueneza sanaa ya muziki nje ya Tanzania na ndani pia.

Hakika “Marehemu hufa na chake” Tuzo zimebaki hadithi yenye masimulizi marefu zaidi na yenye fedheha ndani yake.

Basi upumzike kwa Amani kaka yetu Cool James Mtoto wa Dandu.

Kumbukumbu zako haziwezi kusahaulika mbele ya wajuzi wa muziki, na hakika yaliyo mema huishi kuliko yenye hovyo.

#TuzungumzeMuziki