Mtazamo wa wazi juu ya Young Killer

killer

Mtazamo wa wazi juu ya Young Killer

Popote kambi ni wimbo wake wa mwisho kutoa aliyomshirikisha Mkali Juma Nature, wimbo huu kwangu ni wimbo mkubwa, ila najiuliza kwanini haujapata nafasi katika media kuanzia audio mpaka video?

Young Killer ni moja kati wasanii wazuri wa hiphop kutoka hapa Tanzania, kuanzia uandishi hakika yuko sawa pia katika upande wa flow hakika yuko sawa tena.

Do for me akiwa na Maua Samani wimbo uliotoka kabla ya Kambi popote ya sasa, Lakini wimbo huu wa Do for me hakufanya vyema katika media. Hivyo ni mara mbili mfufulizo amekuja na ujio tofauti lakini bado imeonekana kutokufanya vyema.

Sidhani kama ni nyimbo ambazo hazikustahili kufanya vyema, ila tunaweza kusema katika muziki hutokea mambo kama hayo, wapo waliowahi kutoa zaidi ya nyimbo tatu na wala hazikufanya vyema.

Wasanii wengi hupoteza tumaini hasa anapotoa nyimbo mbili kwa nyakati zinafuatana na wala zisifanye vizuri. Wengi wao hupaniki na kuanza kutoa nyimbo ambazo haziendani na kiwango chake na mwisho wa siku hupotea kabisa.

Young Killer bado anayo nafasi ya kufanya makubwa katika muziki huu wa hiphop, ni vyema kutulia na kutoa kitu bora ambacho kitaendana na ukubwa na heshima yake aliyojiwekea katika nyimbo zako kama, Dear Gambe, Jana na leo, Power, pamoja na nyingine nyingi.

Pia Young Killer anapaswa kujua kutumia zaidi mitandao ya kijamii kupromote kazi yake, iko wazi kama unatumia vyema mitandao ya kijamii basi hakika lazima ukifanyacho kifike mbali. Maana katika miaka hii imeonekana mashabiki walio wengi wanatumia mitandao ya kijamii, hivyo ni wasaa mzuri wa kutumia mitandao ya kijamii kusukuma mbele kazi yako.

Team tizneez inaamini katika kipaji chako, nafasi ya kufanya makubwa katika huu muziki bado unayo, kitumie vyema kipaji bila kusahau Nidhamu!Nidhamu!Nidhamu.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez