Tofauti 4 kati ya Young Killer na Dogo Janja.

Tofauti 4 kati ya Young Killer na Dogo Janja.

Hakuna kosa kufafanisha watu katika Sanaa yoyote ile, ila kosa ni kuwafananisha watu ambao wako tofauti katika mambo mengi yahusuyo Sanaa hiyo.

Mfananisho wa Young Killer na Dogo Janja ni mkubwa na unaendelea kukua siku baada ya siku.

Imani waliyonayo wapenda uchambuzi wa muziki kwetu sisi ni kubwa na maoni juu ya kuzungumziwa jambo la Young Killer na Dogo Janja ni mengi mno. Ila kwa kuwa hatuendeshwi na mtu wala hisia binafsi hivyo tulijipa muda wa kuwasikilzia wote kwa mara nyingi kabla ya kutoa mtazamo wetu ambao wengi wamehitaji.

Ila haaminishi kama hatuwasikilizi bali leo tuliwasikiliza kwa lengo la kujua hasa ni nini au kwanini wanafananishwa kisanaa.

Na ambao wanawafananisha wanafanya katika lengo lipi? Nani mkali katika upande gani? Ingawa jambo hili si baya wala halina dalili ya ubaya kwa vijana hawa.

Kama Team Tizneez tumetazama mambo manne  {4} ambayo hayafanani wala haifai kulinganisha wasanii hawa Young Killer na Dogo Janja.

Jambo la kwanza ni Midondoko, uhalisia Young Killer anabaki kuwa bora katika midondoko kuliko Dogo Janja. Pia Young Killer anabaki kuwa bora maana bado yupo chini ya kivuli cha hiphop, wakati huo Dogo janja haeleweki yuko chini ya kivuli gani. Ila pia hana midondoko iliyo na uzito mbele ya Young Killer.

Uandishi, Hili ni jambo la pili ambalo tumeliona katika mtazamo huu. Ni wazi uandishi wa Dogo Janja ni mwepesi mno ambao huwezi kulinganisha na uandishi wa Young Killer. Nyimbo nyingi ambazo tumesikiliza leo ni wazi Dogo Janja ana uandishi mwepesi usiohitaji kufikirika hata kwa udogo pia uwezo wa kucheza na maneno ni uwezo ambao hana mbele ya Young Killer.

Matumbuizo, ubora wa Young killer katika majukwaa ni mkubwa mno kuliko Dogo Janja.Mara nyingi tumepata kushuhudia matumbuizo yao katika maeneo mengi nje ya leo hii. Umiliki jukwaa wa Young Killer ni mkubwa. Ila yapasa mashabiki wajue mara zote muziki wa hiphop huwa bora jukwaani mbele ya mashabiki. Katika hili huwezi kufananisha kati ya Young Killer na Dogo janja, ni wazi Dogo janja hana uwezo katika majukwaa mengi apandayo.

Kujieleza, Hatua hii ni hatua ambayo huweza kumuinua msanii au kumuangusha katika swala zima la kujieleza katika mahojiano mengi. Swala la kujieleza ni wazi Dogo Janja mara zote huongea kama mtoto ilihali Young Killer kutoa maelezo yenye maana na kuendana na mada husika katika kueleza/kujieleza.

Je!Kuna sababu za watu wa Media kuwafanisha wasanii hawa?

Tupe maoni hapa.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa