Msitumie Chid Benz kupata Likes, Comment na Views

Msitumie Chid Benz kupata Likes, Comment na Views.

Tunajua kila mmoja anatafuta kutrend maana ndiyo jambo zuri katika macho ya wengi.

Na imani kubwa ni kutrend katika hovyo zaidi si mambo mengi yenye mengi na upana wa kueleweka.

Na tunaona mbio zilivyokuwa nyingi wa wahojiji wengi katika upana wa kuhoji mengi yasiyo na maana wala faida kwa msanii.

Tumeona mahojiano ya jana ya Chid Benz kiukweli ni yenye hovyo zaidi. Ni wazi jamaa kwa sasa hayuko sawa na inajulikana.

Kuanza kumuuliza kuhusu madini sijui meno sijui hovyo zaidi haileti maana. Kwanini mtangazaji asingeuliza maswali yenye maana katika kumtafutia msaada zaidi?

Kwa maana ya upo kimya kipi kigumu ambacho unapitia na unapenda labda watu wakusaidie uwe sawa?

Lakini hoji imekaa kimbea katika udhalilishaji, hii maana yake nini?. Ni kwamba imekaa katika mlengo wa kupata Likes, Views na Comment zaidi. (Fedheha)

Lakini nani kasema yakuwa kama angehoji katika upana wa uhalisi wenye maana asingepata hizo Views,Likes na Comment?

Ni kwamba basi tu tupo katika kizazi chenye kupenda hovyo za udhalilishaji zaidi.

Na waswahili hunena yakuwa “Macho hayana thamani kama akili ina upofu”

Sasa kwa semi hii unafikiri watahoji nini kama sio hovyo?. Lakini hatuona la maana katika mahojiano yale zaidi ya fedheha ya udhallishaji juu ya Chid Benz.

Pongezi ziende kwa wote wenye kuhoji yenye maana katika maana na nyakati zenye ukamili.

Soni iwe kwenu wenye kupenda hoji za fedheha katika udhalilishaji. Hakika “Ujinga mzigo”

#TuzungumzeMuziki