Msanii heshimu mahojiano ni mahala pa kuuza bidhaa yako

Msanii heshimu mahojiano ni mahala pa kuuza bidhaa yako.

Kukumbushana na kujuzana mengi yenye  maana katika fanikio la kila mmoja kwenye muziki huu ni jambo jema mno. (Naam)

Inashangaza leo msanii anapata muda wa mahojiano katika chombo chochote cha habari na kuongea hovyo kana kwamba hajui upana wa kuongelea bidhaa yake. (Soni)

Ikumbukwe makampuni makubwa hulipa pesa nyingi mno katika zungumzo la bidhaa yao, tena hupewa muda mchache mno. (Kabisa)

Sasa msanii anapewa zaidi ya dakika 30 na hawezi kuzungumza juu ya bidhaa yake bali yenye hovyo kiasi cha kero kwa wateja wake. (Ajabu)

Muda ambao unapewa na Media uheshimu mno mpendwa msanii, tumia vyema nadi bidhaa yako, isifu kuliko na epuka kuongea yasiyo na maana nyakati umeamua kunadi bidhaa yako. (Umakini)

“Biashara ni matangazo” naam hii ni kwa uhakika, sasa kama biashara ni matangazo msanii anapata wapi muda wa kutangaza yenye hovyo zaidi wakati wa kunadi bidhaa yake? (Ulizo)

Mahojiano yanaweza kuangusha biashara ama kupandisha na hii kutokana na namna ya uzungumzaji wa msanii. (Uhalisia)

Mfano hai ni Godzillah baada ya mahojiano yake na Xxl ya Clouds Fm yameleta matunda gani katika uuzo wa bidhaa yake? (Fedheha)

Hakuna zaidi ya wateja wake na wengine kuona ni mtu mwenye mfadhaiko zaidi huku mengi yenye uropokaji nje ya bidhaa yake yakitawala kinywa chake. (Soni)

Lakini muda ule alipaswa kunadai bidhaa yake kwa upana hakika ingempa matokeo mema maana katika uwazi watu wa kiu na bidhaa za Zillah. (Eeh)

Lakini nini kimetokea baada ya mahojiano yale? ni anguko jema ambalo Zizi hana wa kumlaum zaidi ya yeye mwenyewe. (Yeye)

Msanii/wasanii ni vyema mjue mahojiano ni mahala pa uuzo wa bidhaa zako kwa upana, yatumie vyema. (Naam)

#MuzikiNiSisi