Mrisho Mpoto vua vazi la unafiki na sifa mbele ya jamii. (Soni)

Mrisho Mpoto vua vazi la unafiki na sifa mbele ya jamii. (Soni)

Kivazi cha unafiki ni wazi kimemvaa kaka yetu Mpoto na kimemtosha vyema mbele ya wajuzi imara. (Kabisa)

Na unafiki umepingwa hata katika vitabu vya dini lakini hata katika uisho wetu sisi waswahili imara. (Hakika)

Daima sifa ya kwanza ya mnafiki ni kujivika vazi la wema mbele ya jamii iihali anajua yakuwa anatenda yaliyopotoka. (Eeh)

Na tunapenda mjue yakuwa Unafiki ni “utovu wa ukweli katika mwenendo wa ubinadamu hasa kwa mlengo wa kujikombea sifa”. (Ajabu)

Mnafiki hutenda unafiki ili kujikombea sifa zaidi mbele ya watu ili kupata faida fulani kutoka kwao. (Mnafiki)

Ni aibu kuona eti unamjuza Diamond Platnumz kuhusu msiba wa Ruge kiasi aende akamzike. Kama kweli nia yako ni njema kwanini usipige simu yake? (Ulizo)

Kweli mtandao wa picha ‘Instagram’ iwe ni sehemu ya kumpa Diamond habari juu ya msiba wa Ruge? (Soni)

Kweli Diamond hajui kuhusu msiba huu? (Anajua). Lakini hakuna lazimisho juu ya yeye kuonesha yakuwa ameguswa au ulazima wa kumzika Ruge ama kutoa heshima yoyote ile. (Ndiyo)

Lakini hakuna ambaye hajui na hatojua nafasi ya Ruge katika muziki wa Diamond na wasanii wengine wengi zaidi. (Katengeza)

Baada ya posti ya Mpoto ni wazi wapo ambao watakutafuta wakuhoji kwa upana na utapata mahojiano mengi zaidi, lakini ni wazi kwa taarifa eti Diamond aje amzike Ruge umepotoka. (Soni)

Ni nani ambaye hajui kama Ruge Mutahaba amefariki? ni yeye Diamond Plunumz pekee yake ama? (Ajabu)

Ilihali serikali yote inajua, balozi zote za nchi mbali mbali zajua itakuwa Diamond? na vyombo vyote vya habari vikiripoti nyakati zote tangu kifo chake mpaka sasa, sa ni kipi ambacho kimekupa mshawasha na kuandika ujumbe soni mtandaoni? (Kiki)

Ifike mahali watu mpate kuwaza kwa upana, hakuna ulazima wa Diamond kulizimishwa kusikia uchungu au kuweka posti, kwa maana msiba undani ya mtu. (Uhalisia)

Kwa semi ya mpoto maana yake ni kwamba Ruge hawezi kuzikwa bila Diamond? (Chekesho kubwa). Mrisho Mpoto ni wazi heshima yako umeishusha mno kwa mambo ya kitoto katika mtandao. (Upuuzi)

Na daima “Mtu mzima akivuliwa nguo hadharani huchutama” (Hakika). Na hakika wimbo wa Wagosi wa Kaya wa Sifa za kijinga ukufikie. (Ujinga)

 

Tazama posti yake Mpoto kutoka kwenye mtandao wa Picha ‘Instagram’

 

#MuzikiNiSisi