Mr II Sugu ni alama ya bora ya muziki wa bongo fleva/hiphop nyakati zote.

Mr II Sugu ni alama ya bora ya muziki wa bongo fleva/hiphop nyakati zote.

Ni sisi wenye kusema haya maana yapo ndani yetu, nasi si wale wa kupangiwa hata cha kuandika kama walivyo wengi.

Nyakati zote husema kweli yenye kweli, kwa mengi aliyotenda Mr II Sugu kwenye huu muziki hakika yapasa aheshimiwe nyakati zote.

Tukisema Sugu ni chachu ya maendeleo na ukombozi wa huu muziki, hakika hakuna wa kupinga hata kwa udogo.

Sugu alikuwa mtu wa kwanza kudai haki za wasanii katika ngazi zote, shoo na mirabaha.
Lakini kuwafungua wasanii juu ya kuacha kuwa watumwa wa Media/Wadau na kutaka ujira wao kabla ya kutumika.

Hivyo unavyoona sasa wasanii wakiwa vifua mbele katika kweli yao, hakika chanzo kikuu ni Sugu ambaye sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini.

Ingawa imekuwa ni desturi sasa kusema kweli yenye kweli mtu akiwa hayupo hai, bali akiwa hai watu hufunga vinywa vyao. (Unafiki)

Leo ni kumbukumbu yake ya tarehe na mwezi katika uzao wake kaka yetu Sugu, hivyo kwa heshima yake katika huu muziki tumeona yapendeza tunene mambo kadhaa juu yake.

Hasa album yake ya kwanza ambayo yaitwa ‘Ni Mimi’ ambayo ilitoka mwaka 1995.Na ilikuwa na nyimbo takr ibani 9 na album hii iliandaliwa na Marlon Linje katika Studio za Don Bosco.

Na utengenezaji midundo Marlon Linje alisaidiwa na Willy na Terry ambao ni waasisi wa kundi la Hardblasters. Na ushiriki wao ulikuja maana Linje hakuwa na uwezo wa kutengeneza midundo ya hiphop.

Na album hii ilitumia kiasi cha 44,000 kama gharama uandaaji, na album ilikamilika rasmi na kutoka mwaka 1995.

Na album hii ilikuwa na nyimbo hizi
1. Ni Mimi Feat Terry
2. Ya oh yanatisha
3. Blood Shed
4. Kesho kwa Mungu
5. Instrument
6. Siku
7. Ni wapi?
8. Siku (Ext. Version)
9. Ni Mimi (BassMix)
10. Shootout

Usikilize/tazama wimbo wa NI MIMI uliobeba jina la album hii


Lakini Sugu ndiye msanii ambaye anaongoza kwa album katika muziki wa kizazi kipya, mpaka sasa ana album 10.

Team nzima ya Tizneez inakutakia kheri katika kumbukumbu yako ya uzao na muendelezo mwema.

#TuzungumzeMuziki