Mr Blue ni yeye na muziki wake.

Mr Blue ni yeye na muziki wake.

Ni wazi wasanii wengi ni watu wa mambo mengi katika udaku ambapo kama wengi wangekuwa ni wafuatiliaji wa muziki ni wazi tusingeweza kuwafahamu kabisa.

Wapo wasanii wengi mno ambao daima wao ni kelele katika mengi hasa yaliyo nje ya muziki. Lakini yafaa mjue yakuwa “Mwenye kelele hana neno”.

Lakini “Mtembea peku hapendi ila hana viatu” (Kipaji)

Mr Blue si msanii wa kelele kabisa katika mambo yasiyohusu muziki, bali utulivu na kusimama vyema na muziki wake.

Ila kelele zake ni pale ukimpa kipaza mbele ya mashabiki kwa hakika hapo utaona kelele zake lakini kelele za mashabiki. Muziki haujabadilika kama wasemavyo wengi, bali wasanii ndiyo wamebadilika katika kuufanya maana hawaamini katika muziki pekee ila zaidi yake.

Mr Blue ni yule yule na muziki wake na tumeona akifanikiwa vyema katika uwanja wa muziki.

Na waswahili husema ” “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu, Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi”

Ni wazi nidhamu ya kusimama na muziki wake itaendelea kumuweka vyema katika muziki huu wakati wote.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa