Mr Blue Mbabe wa muziki asiye na kelele.

Mr Blue Mbabe wa muziki asiye na kelele.

Hakika “Atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu” (Hakika)

Semi hii inatupa upana wa tazamo kuu kwa Mr Blue yeye si mtu wa mambo ya aibu bali uhalisi wa kazi yake katika pole na tulivu imara. (Ndiyo)

Tunapenda tuwajuze katika kweli yenye kweli kutoka kwa wajuzi yakuwa “Mr Blue ni msanii bora wa nyakati zote” (Eeh)

Kuimba na kuchana vi ndani ya uwezo wake tena kwa usawa wa ujazo wa wa juu kabisa, na hii ni katika fanya ya muziki atakavyo. (Uhalisia)

‘Blue’ huu ni wimbo wa kwanza kutoka kwake Mr Blue kwa mwaka 2019 na hakika ni wimbo bora katika upana wa wimbo kamili. (Naam)

Sauti za nyuma ya wimbo huu wa ‘Blue’ kutoka kwa Nandy unaleta nogesho la ladha tamu ya usikivu. (Sikio)

Mitambo ya taratibu na majigambo yenye uhalisi kutoka kwa Mr Blue inaleta chocheo la kusikia neno kwa neno ilihali mstari kwa mstari. (Michoro)

Ila namna ya kubadili mitambao kila baada ya mistari kadhaa inafanya uone upana wa ukomavu wa Blue katika kucheza na muziki afanyayo vile atakavyo. (Ndiyo)

Lakini pia mdundo wenye vionjo kamili katika dundo unaweka hitimisho la wimbo kamili katika ubora imara. (Hakika)

Licha ya ubabe katika kazi zote katika ubora lakini Mr Blue si msanii mwenye kelele katika mengi yenye mengi. Yeye ni kuuza bidhaa yake ya muziki tu si mtu wa lawama wala malalamiko hata kwa udogo. (Upana)

Na daima hata mswahili hunena yakuwa “Mwenye kelele hana neno” (Naam) Hakika Mr Blue ni mbabe kwenye muziki asiye na kelele, wimbo huu wa Blue umefanya endelezo la ubora wake. 

Hakika ni wimbo bora wenye ubora kamili wa wimbo, Kuna yoyote mwenye kupinga ubora wa wimbo huu? (Hayupo)

#MuzikiNiSisi