Mpishano wa Ruby na muziki katika usawia wa nyakati kamili.

Mpishano wa Ruby na muziki katika usawia wa nyakati kamili.

Nyakati zote twanena yakuwa Ruby ni moja ya waimbaji bora ambao wanapaswa wapewe nafasi kubwa kulingana na ukubwa wa kipaji chake. Ni wazi mengi yametokea katika muziki wake, na miluzi mingi ni moja ya upotevu, Hasa katika changanyo la uimbaji singeli.

Na singeli ni mpishano wa Ruby na muziki katika ile kweli yenye kweli ndani ya nyakati kamili. Hakika ile haikuwa njia yake, ila haraka na kuyumbishwa lakini kujiyumbisha ndicho chanzo kikuu.(Fedheha) .

Na wajuzi wa muziki hunena yakuwa “Sio kila msanii anaweza kufanya aina zote za muziki” wapo ambao hushindwa, na muziki si sanaa ya kujaribu katika bahati, bali kufanya kwa uhalisi wako msanii.

Na ndiyo maana ya ‘muziki’ ni hisia, hivyo yapasa msanii apende kwanza aina nyingine ya muziki ndiyo aweze kufanya vyema, maana kupenda huanza na hisia.

Je!Ruby alipenda kwanza singeli kabla ya kufanya? au ni katika ulazimisho? ni vyema tuwe tunafikiri. Na sasa upo Niwaze ambao ni wimbo wake Ruby akiwa na The Mafik,hakika amefanya katika kiwango cha juu, lakini The Mafiki pia.

Nani aliwaza ujio huu? wengi walijua Ruby ataenda na upepo uliopo katika muigo wa makapuka mengi, ambayo hayaonyeshi ujuzi wa uimbaji wa msanii.

Lakini kujua muziki ni hisia kumefanya Ruby arudi katika njia yake, na mswahili anena yakuwa “Hekima ni kupaza sauti katika njia kuu”

Naam! hii imeonyesha yakuwa Ruby bado hana wa kulinganishwa nae usawa wake kwenye swala zima la uimbaji. Na hizi ni nyakati kamili za Ruby licha ya mpishano wa muziki katika nyakati fulani.

#TuzungumzeMuziki