Mpaka sasa tuna wasanii wanne marehemu ambao wameacha album zao zikiwa hazijatoka.

Mpaka sasa tuna wasanii wanne marehemu ambao wameacha album zao zikiwa hazijatoka.

Mswahili hunena yakuwa “Kifo na kiumbe, kiumbe na kifo” Lakini hakuacha kunena yakwamba “Chochote chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo”

Kwa nyakati zao wasanii hawa wote walitimiza vyema, ambapo Albert Mangweir alifariki mnamo 25.5.2013 nchini Afrika ya Kusini na kuzikwa nyumbani kwao Morogoro.

Na swaiba wake M To The P amethibitisha yakuwa mwaka huu album yake itatoka.

Wakati huo Geez Mabovu alifariki 12.11.2014 Mkoani Iringa na kuzikwa Iringa nyumbani kwao.

Na Lamar amethibitisha yakuwa anayo album ya Geez Mabovu ambayo alirekodi tangu 2007 na haijatoka.

Na mkali mwenye asili ya kimasai Mr Ebbo yeye alifariki 1.12.2011 Jijini Arusha na kuzikwa Arusha. Ambapo Jeff ambaye ni muongozaji wa video takribani zote za Mr Ebbo anathibitisha yakuwa anayo album ya Ebbo pia.

Kadhalika Langa ambaye alifariki 13.6.2013 Jijini Dar Es Salaam, na kuweza kuzikwa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wajuzi lakini msanii mwenzake na rafiki yake wa karibu Wakazi anathibitisha yakuwa album ipo na haijawahi kutoka.

Na wajuzi wanaamini yakuwa katika nyakati hizi muziki ukiwa umechangamka kwa soko la album wasanii hawa album zao zikitoka zitauza vyema.

Ni kwa maana ya mashabiki wengi kutamani kusikia nyimbo mpya za wasanii hawa. Hivyo wajuzi wananena yakuwa ni vyema na ni muda sahihi kwa watu wenye album za wasanii hawa kutazama kwa upana namna ya kutoa album hizo na kuuza vyema.

#TuzungumzeMuziki