Mnataka Grace Matata afanye jambo gani mpate kujua thamani yake?

Mnataka Grace Matata afanye jambo gani mpate kujua thamani yake?

“Grace matata ni farasi anaepitwa na kinyonga”ni jambo la kushangaza mno katika wasanii wa kike ambao wana vipaji vya hali ya juu sasa kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya jina la Grace Matata halipo kabisa. Licha ya kuwa bora Zaidi ya wale ambao unawasikika kila leo kwenye vituo vingi vya radio/Runinga/Blog/Magazeti (Media)

Kujiuliza maswali juu ya Grace Matata ni tendo linalojirudia mara kwa mara pale tu ninapofungua radio/Runinga na kusikia/kutazama mtangazaji akisifu uwezo wa wasanii wengine wakike bila kutaja kabisa jina la Grace Matata.

Imani ya bila media inawezekana si jambo la kulipa nafasi kwa sasa, katika uhalisia bado kuna ugumu mkubwa katika nchi yetu.Ya nini tuupe uongo nafasi?nguvu ya media bado ni kubwa mno, licha ya mitandao kuwepo ila nguvu ya mitandao ni kubwa kama itatumika kikubwa.

Media ikiamua hiki kiwe hivi ni wazi kitakuwa kilivyo. Jambo hili halina ubishi mfano tosha wa media kuamua jambo ni mfano hai wa Harmorapa.

Ilianzia kwenye media ndio ikafika kwenye mitandao ya kijamii, hivyo media ilikuwa daraja zuri la watu kufahamu kuhusu Harmorapa.

Ubora wa Grace Matata ni tangu pale alipotoa album yake ya kwanza ya Nyakati miaka ya 2014, ambapo album hiyo iliuzwa kwa njia ya mtandao tu.

Nyimbo kama Free soul,Nyakati,utanifaa,hellow,na nyingine nyingi zimeweza kudhihirisha ubora wake mbele ya wadada walio wengi ambao hawafikii hata robo ya uwezo wake isipokuwa ujanja wa kucheza na akili za watu wachache wenye kuseti ‘trend’juu ya upuuzi ……. Itaendelea

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa