Mnataka Grace Matata afanye jambo gani mpate kujua thamani yake? Sehemu ya II

Soma sehemu ya kwanza hapa.  http://tizneez.com/makala/mnataka-grace-matata-afanye-jambo-gani-mpate-kujua-thamani-yake/

Zaidi na sio nyimbo nzuri.

Hii imekuwa ni tamaduni mbaya sasa kwa watu wa media, ni jambo endelevu sasa wale ambao hawana uwezo kupewa nafasi Zaidi.

Ya nini tuukumbatie uongo, ilihalia ukweli utatuweka huru. Ipo mifano mingi katika hili la watu kuamua kuwakalia kimya wenye vipaji halisia na kuamua kuwapa nafasi watu wenye vipaji vya kulazimisha. Sijui ni kwanini lakini.

“Iseme ile kweli yenye kweli itakayoleta ukweli maishani” Amber Lulu ni moja kati ya vipaji vya kulazimisha kwenye muziki, ila katika upande wa kuwa ‘video vixen ‘ yuko sawa. Ila muziki hapana ni wazi anachosifiwa sicho alichonacho, uongo wa nini? Tukisema ni rushwa, fitna,chuki,na urafiki nani atapinga? Nikitoa Amber Lulu wapo wasanii wengine wengi mno ambao hupewa sifa wasizonazo kwenye muziki.

Nishapata wasaa mwingi wa kuwa katika matamasha mengi ya muziki wa kizazi kipya, Grace Matata anabaki kuwa bora katika jukwaa. Ila pia anabaki kuwa bora katika uandishi, anabaki kuwa bora katika uimbaji, anabaki kuwa bora katika Sanaa ya muziki. Ila haya mbona hayasemwi?

Watu wanahitaji afanye nini ili tuone ukubwa na thamani ya kipaji chake?

‘Ukiipa nafasi akili kuongea, mdomo utashangaa’ Ipo kila sababu ya kuipa nafasi akili juu ya kubadili mitazamo ya kuvipa nafasi vipaji visivyo stahili, bali tuvipe nafasi vipaji stahili.

Jambo hili litakuza kwa kasi muziki wetu wa kizazi kipya maana tutakuwa na wasanii walio bora katika mambo yote, kuanzia jukwaa,Utunzi,Uiambaji,Nidhamu na kila lenye uhitaji kwenye Sanaa ya muziki.

Umefika muda sasa wa kumtazama Grace Matata. Tusitazame maslahi binafsi bali maslahi ya muziki wote kwa ujumla.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

 

Mwisho.