Mnashangaa ya Fey? mmesahau ya Gigy Money na Amber Lulu?.

Mnashangaa ya Fey? mmesahau ya Gigy Money na Amber Lulu?.

Hakuna awezacho kufanya Fey zaidi ya akifanyacho sasa, na ni wazi kimempa tokeo jema.

Wakati lugha kali zikiendelea juu yake, huku wengine wakiona anavuka mipaka zaidi hivyo yapasa vyombo husika vichukue hatua kali.

Lakini sisi washamba na wazungumza muziki tunawauliza kwanini muone shangazo kwa Fey?.

Mbona ni wepesi mno wa kusahau? leo hii tayari mmesahau ya Amber Lulu na Gigy Money? (Soni)

Kwani wao walianza na yepi? mema? au simamio la muziki?. Ni vyema mkumbuke kumbukumbu, ni lazima Fey afanye kuzidi wale ili achukue soko kwa upana.

Na sasa tunaamini kwa hakika “Kwa wajinga ndiyo kuna hela”. (Upuuzi).

Tangu Fey aanze kufanya ya hovyo amepata mahojiano mengi mno tena kwa upana wa hali ya juu.

Ingawaje kwa wenye utashi huona chukizo katika hoji zake nyingi apewazo, lakini wenye utashi wanashinda wajinga ambapo ndipo upande wa hela?.

Mwacheni Fey aishi katika dunia ya wengi yenye njia ya urahisi kwa kuweza kufikia mafanikio ya muziki.

Maana muda mchache ufuatao wimbo wake utatoka, na atakula faida nzuri. Ni wazi sasa yukatika matangazo mema.(Uhalisi)

Hivi mmevikwa upofu wa Gigy Money na Amber Lulu katika muziki sasa? si wanafanya vyema? je! njia zao zilikuwa zipi?. (Chekesho)

Eeh! basi msishangazwe na Fey maana “Vya kurithi vinazidi nyakati zote”

Bado mnataka kushangaa ya Fey tena? hakika mtakuwa ni wenye tatizo, muacheni achagize awezavyo.

Na tegemeo ni fanikio katika muziki maana imekuwa ni njia rahisi tu ukitaka kutoka kimuziki basi tenda ya hovyo kwa mapana.

Hakika tutaona akina Fey, Gigy na Amber Lulu wengi zaidi, nyakati zimefika. Mbegu ya hovyo imepandwa na itaota hovyo kwa mapana ya hovyo.

Na daima “Kuwasha taa kwa pofu ni kuharibu mafuta”. Sasa mnataka elimisho kwa Fey? yani tunene sisi washamba wa muziki? Jamani tutapoteza nyakati tu.

Fey endelea na tenda zaidi ya zaidi maana faida yake ni kuu, ilihali chukizo ni kubwa mno. Wenye kushikilia muziki si wengi, naam! wengi ni matendo basi yatende tena na tena yani tena tenda.

La!hasha hovyo yakera kwa ukubwa, lakini aminini twanena “Kwa wajinga ndiyo kwenye hela” kwani hamuoni?.

Fey endeleza hovyo soko linataka hovyo basi wape hovyo tena tunakwambia utapata mahojiano ya kutosha, maana wahoji nao ni hovyo.

Hovyo na hovyo huleta biashara imani yao yaamini hivyo, basi tenda hovyo kwa upana wa hovyo.
Tafakarii….