Mjinga asipoelewa jambo hugadhibika,lakini mwerevu hukuna kichwa (EATV AWARDS 2016)

me

Mjinga asipoelewa jambo hugadhibika,lakini mwerevu hukuna kichwa (EATV AWARDS 2016)

‘Mwenye sifa yake mpe’ imekuwa jambo baya kwa wengi kusifu uhalisia wa kitu fulani hata kama ni kizuri. Lakini ukitazama kwa umakini kwanini hasifu ukweli uliopo ni wazi ameweka mbele hisia zake ambazo hazina maana wala faida katika maisha ya kuendeleza kujenga muziki huu wa kizazi kipya.

Team tizneez tunachukua nafasi kuipongeza Team nzima ya Eatv Awards kwa kuandaa jambo hili na hakika limeta chachu ya kurudisha umuhimu wa tuzo za nyumbani, lakini pia kuweza kuiuganisha Afrika Mashariki kimuziki kwa ujumla katika tuzo hizi. (Pongezi)

Hakuna jambo lisilo na malalamiko hasa katika maswala ya utoaji tuzo. Ni wazi kila shabiki anatamani msanii wake ndiyo awe mshindi, hivyo changamoto hii ipo katika kila tuzo duniani.

Ila moja ya hoja kubwa  iliyoko zaidi kwa baadhi ya mashabiki wa Diamond Platnumz pamoja na team yake nzima ya Wasafi ni kwanini hawaja onekana katika mchakato wa tuzo hizi. (Ushiriki)

Malalamiko haya yanatolewa katika lugha kali mno, lakini sio lugha kali tu hata kusema kuwa Diamond na team yake ni wakubwa kuliko tuzo.(Ama kweli fahari mama wa ujinga) Hoja hizi nazitazama katika mlengo wa kushangaa mashabiiki hawa.

Lakini siachi kupata majibu ya hoja zao kwa kutumia hekima za misemo ya wahenga. ‘Huwezi kuona msitu ukiwa msituni’. Watu hawa wana kila sababu ya kutoa hoja zao zisizo na mashiko. Maana wengi wao wapo kwenye msitu. Maana mara zote ni watu wa kutumia lugha kali bila hata kutaka kuchukua muda wake kufuatilia jambo kwa kina.

Tuzo hizi zimekuja na utaratibu wake, hivyo lazima uheshimu utaratibu huo. Moja kati ya utaratibu ambao uliwekwa ni msanii kujaza fomu ya ushiriki,hivyo ni wazi kama msanii hajajaza fomu na kurudisha hawezi kuwekwa katika tuzo hizi.

Huenda ukawa ni utaratibu mpya lakini hatupaswi kuupinga maana ndiyo utaratibu wao ambao wao wameona inastahili kuwa hivyo ilivyo. Ila pia si jambo baya kutoa maoni ila maoni yakiltolewa katika lugha nzuri ni wazi yanaweza kutumika vyema.

Leo hii msanii yoyote akitaka wimbo wake uchezwe katika vituo vikubwa kama Mtv, Trace na nyinginezo ni lazima ajaze fomu za maombi ya kuomba wimbo wake uchezwe. Wasanii wote wanajaza fomu hizo, lakini kama ingekuwa ni katika Media za hapa tungeona ni dhambi kubwa.

Huo ni utaratibu wa hizo Media.Cha ajabu wasanii wote wanafuata bila hata chembe ya lawama. Sina hakika na mashabiki hewa kama wanajua hili.

Sasa kama wanaweza kufuata utaratibu wa media za nje kwanini washindwe hapa ndani tena kwa media zilizofanya wajulikane!!

Yapasa mjue ‘Huwezi kwenda kwa jirani pasi kutokea kwako’ hivyo wasanii wote wanakila sababu ya kuheshimu tuzo hizi.

Lakini katika uhalisia media za nje hazina nguvu katika soko la muziki la ndani.

Pongezi kwa kila aliyeshiriki pia pongezi kwa washindi wote wa tuzo hizi.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa