Milango ya kuziona Taasisi za Sanaa kwanini imefungwa kwa Roma Mkatoliki?

Milango ya kuziona Taasisi za Sanaa kwanini imefungwa kwa Roma Mkatoliki?

Hilo ni swali kuu kwa watu wengi na wasomaji wa Tizneez, kwa hakika tumeulizwa mara nyingi.

Lakini nasi hatuna majibu juu ya swali hilo maana nyakati tulizopo ni nyakati za wengi kuhubiri mengi ambayo hawayatendi na ukweli kuwekwa nyuma. (Upindishwaji)

Na waulizaji maswali kwetu sisi, pia sisi mioyo yetu imejaa maswali mengi juu ya Taasisi za Sanaa zote ambazo zina mamlaka kisheria.

Maana ni wiki moja tu imepita pale ambapo Roma Mkatoliki alipofanya mahojiano katika kipindi cha XXL kwenye kituo cha Radio Clouds Fm.

Ambapo katika mengi aliyosema moja wapo ni “Mimi, Madee na Askofu tulienda ofisini kumuona Mh Naibu Waziri, wenzangu waliitwa pekee yao. Mimi nikaambiwa sina ruhusa ya kwenda kuingia ndani, ningefanyaje? Na huwezi kulazimisha kuingia”.

Na katika kweli ni wazi Roma alifuata taratibu zote ili kuweza kuwaona wahusika wa Taasisi hizi za Sanaa. Kiasi cha kutumia mpaka chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Tuma) Tanzania Urban Music Assocition.

Lakini Roma juhudi hizi ziligonga mwamba na kushindwa kuwaona wahusika wa Taasisi hizi za Sanaa ili kuweza kuwasilisha kilio chake na wasanii wengine ambapo alipaswa kuambatanao.

Lakini imekuja kwa upande wa Diamond Platnumz aliongea kwa upana kwenye kipindi cha Playlist cha Times Fm, lakini baadae kwenye mtandao wa Twitter kupitia ukurasa wake aliweza kuandika vingi ambavyo vilileta sintofahamu kwa ukubwa mno.

Na hata viongozi wa Taasisi walijibu hoja zake Diamond na hakika zilizidi kuleta mkanganyiko wa hali ya juu.

Hisia za wengi zilikuwa ni kuwepo kwa ukakasi mkubwa juu ya Diamond na Taasisi za Sanaa baada ya kuongea kauli ambazo wengi walizitazama kami dharau mbele ya viongozi hawa wa Taasisi.

Lakini haikuwa hivyo maana ni wazi jana amepata kumbatio jema na Taasisi, ilihali Taasisi husema nyakati zote hazifanyi kazi na msanii mmoja mmoja bali tasnia nzima. Je!imekuaje sasa kwa Diamond pekee?

Lakini tukimtazama Roma ambaye yeye aliitafuta hii nafasi kwa muda mrefu na kuikosa, iweje Diamond aipate kiurahisi Zaidi? Hii inatoa maana gani kwa Roma na wasanii wengine?

Wakati huo Taasisi husema hawafanyi maamuzi na msanii mmoja bali tasnia nzima, hivyo wanataka kuaminisha kuwa Diamond pekee ndiyo tasnia nzima?

Sasa mbona aliyetumia chama cha muziki kama Tasnia nzima kushindwa kupokelewa au kusikilizwa? Na huyu aliyekuja pekee kusikilizwa na kupewa kumbatio?

Hii inaonyesha wazi Taasisi kushindwa kuishi katika maneno yao yakuwa hawafanyi kazi au maamuzi na msanii mmoja mmoja bali jumla.

Na ikumbukwe Roma amefungiwa asijihusishe na kazi ya Sanaa kwa miezi 6, na Sanaa ndiyo kazi yake tegemezi ya kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla.

Lakini aliyefungiwa nyimbo 2 na kuendelea na kazi ya Sanaa ndiye mwenye kusikilizwa Zaidi, hakika hii haileti maana.

Na uzalendo wa ubaguzi ndiyo mbegu ipandwayo vyema katika shamba la mashabiki na wasanii kwa ujumla. (Taasisi)

Na nyakati zote huwa yakuwa “Mwenye haki huyaangalia madai ya masikini, bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue” Je!Taasisi zimekuwa ni watu wabaya?

Mbona haziangalii madai ya wasanii masikini kama akina Roma? Hii maana yake nini? Au ndiyo tunaishi katika semi ya mswahili yakuwa “Mwenye moja havai mbili”

Tafakari…!

Itaendelea…….!!!

 

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa